Burudani

Wizkid na Eddy Kenzo watikisa jukwaa la One Africa Music Festival Marekani, Diamond na Davido waingia mitini (+video)

Wikiendi iliyopita nchini Marekani kulikuwa na tamasha kubwa la One Africa Music Festival 2018 linakutanisha mastaa kibao wa muziki kutoka barani Afrika.

Tamasha hilo lilikuwa na orodha ndefu ya majina ya wasanii kutoka Afrika akiwemo Tekno, Davido, Diamond Platnumz, Casper Nyovest, DJ Spinal, Vanessa Mdee, Eddy Kenzo, Wande Coal, Sarkodie, Mr. Flavour, Kizz Daniel na wengine kibao.

Kitu cha kushangaza licha ya awali waandaaji wa tamasha hilo kutangaza majina mengi ya wasanii lakini mwisho wa siku waliohudhuria wahajafikia hata nusu ya wasanii waliotajwa.

Awali majina yote ya wasanii waliotumbuiza mwezi uliopita jijini London kwenye tamasha hilo ndio waliokuwa wametajwa kutumbuiza tena Jumamosi iliyopita jijini New York .

Diamond Platnumz, Davido, Vanessa Mdee, Kizz Daniel ni moja ya wasanii ambao licha ya kutangazwa awali kutumbuiza kwenye tamasha hilo lakini hawajaonekana kwenye jukwaa na tayari  wasanii hao wamefuta posti zote za tamasha hilo kwenye kurasa za mitandao yao ya kijamii.

Hata hivyo waandaaji wa tamasha hilo licha ya kupiga nyomi wamejikuta wakishambuliwa kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii kwa kushindwa kutolea maelezo kwa baadhi ya wasanii kushindwa kutumbuiza kwenye jukwaa hilo.

Mpaka sasa hakuna taarifa rasmi za waandaaji hao kuhusu kukosekana kwa mastaa hao wa muziki. Kama kawaida Afrika Mashariki tuliwakilishwa na Eddy Kenzo kutoka Uganda na show ilifanyika kunako ukumbi wa Ford Amphitheater,  Brooklyn jijini New York. Tazama show ya Davido na Eddy Kenzo

https://youtu.be/uMCiDk9neEM

https://youtu.be/eJ0YNS06E2s

Related Articles

10 Comments

  1. Salim Pesa umeambiwa wasanii wote ambao hawakutokea ila walialikwa baadae walifuta post za tamasha kwenye page zao on social media umejua ni kwa nini? Fuatilia Kaka then ndo useme linalokukela sio kukalia mvaa kikuku hapo utachelewa sana bro kumfuatilia SIMBA na nyendo zake! league kuu Tanzania bara nadhani inaanza muda si mrefu jipange Mzee Baba kushangilia Coastal Union jamaa yuko pale anakipiga!! Huku kwenye vikuku usije ukajaribu unaweza ukajikuta na wewe unavaa!!

  2. Wizkid na Eddy Kenzo watikisa jukwaa la One Africa Music Festival Marekani, Diamond na Davido waingia mitini (+video)

    Godfrey Mgallah 11 hours ago

    878

    Wikiendi iliyopita nchini Marekani kulikuwa na tamasha kubwa la One Africa Music Festival 2018 linakutanisha mastaa kibao wa muziki kutoka barani Afrika.

    Tamasha hilo lilikuwa na orodha ndefu ya majina ya wasanii kutoka Afrika akiwemo Tekno, Davido, Diamond Platnumz, Casper Nyovest, DJ Spinal, Vanessa Mdee, Eddy Kenzo, Wande Coal, Sarkodie, Mr. Flavour, Kizz Daniel na wengine kibao.

    Kitu cha kushangaza licha ya awali waandaaji wa tamasha hilo kutangaza majina mengi ya wasanii lakini mwisho wa siku waliohudhuria wahajafikia hata nusu ya wasanii waliotajwa.

    Awali majina yote ya wasanii waliotumbuiza mwezi uliopita jijini London kwenye tamasha hilo ndio waliokuwa wametajwa kutumbuiza tena Jumamosi iliyopita jijini New York .

    Diamond Platnumz, Davido, Vanessa Mdee, Kizz Daniel ni moja ya wasanii ambao licha ya kutangazwa awali kutumbuiza kwenye tamasha hilo lakini hawajaonekana kwenye jukwaa na tayari wasanii hao wamefuta posti zote za tamasha hilo kwenye kurasa za mitandao yao ya kijamii.

    Hata hivyo waandaaji wa tamasha hilo licha ya kupiga nyomi wamejikuta wakishambuliwa kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii kwa kushindwa kutolea maelezo kwa baadhi ya wasanii kushindwa kutumbuiza kwenye jukwaa hilo.

    Mpaka sasa hakuna taarifa rasmi za waandaaji hao kuhusu kukosekana kwa mastaa hao wa muziki. Kama kawaida Afrika Mashariki tuliwakilishwa na Eddy Kenzo kutoka Uganda na show ilifanyika kunako ukumbi wa Ford Amphitheater, Brooklyn jijini New York. Tazama show ya Davido na Eddy Kenzo

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents