Burudani

Wizkid na Runtown waingia kwenye chati za Billboard Twitter Top Tracks

Wimbo wa Wizkid ‘Daddy Yo’ na ule ya Runtown ‘Mad Over You’ zimefanikiwa kuingia kwenye chati za Billboard Twitter Top Tracks chart ya Marekani.

‘Daddy Yo’ umefanikiwa kushika namba 31 huku ‘Mad Over You’ ukishika namba 38 kwenye chati hizo.

Hii ni mara ya pili kwa Wizkid kuingia kwenye chati hizo baada ya kuingia kwa mara ya kwanza kupitia wimbo wa ‘One Dance’ alioshirikishwa na Drake lakini kwa Run Town hii ni mara yake ya kwanza.

Baada ya kuingia kwenye chati hiyo, Runtow aliandika kupitia mtandao wa Instagram, “Thank You #TeamRuntown #TeamSoundgod ,Let’s make it Number One ❤️ @billboard.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents