Bongo Movie

Wolper anahofu na ‘nyakunyaku’ kwa bff wake?

Msanii wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper ameonyesha kuanza kuwa na hofu kwa baadhi ya marafiki ambao wanatabia ya kuchukua wapenzi wa watu.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, mrembo huyo ameandika kuelezea jinsi aliyoamua kuanza maisha mapya ya kimapenzi na kuelezea drama zilizopo katika mahusiano.

Yani bwana nimekaa nimewaza hapa mwenyewe!Mahusiano siku hizi yamekuwa yana Drama mno,Leo huyu kachanganywa na shoga ake,kesho ukiachana na huyu shoga ako yupo nae,Mara unaletewa wote mnafanganywa mtaolewa mwisho wa siku mnaambulia maumivu na majuto!Hii sana sana inatukuta sisi wadada,Yani wanaume wanatuchezea akili km mpira vile!Na sisi wadada nao maskini uwezo wa kufikiria mdogo tukigombana mwanaume akija na vizawadi tu,tunasahau maumivu na usaliti wote ??Kwa mfano mm nimesha experience hayo yooote yani kiasi kwamba sioni jipya ktk mahusiano,Na ndio maana nimeamua nianze upya lifestyle yangu!yani tukipendana sawa ila ukizingua sina mda wa kuvumilia matatizo (Yaaaani nakumwaga) Kuliko kufanywa mtoto kuchezewa akili mtu hauwazi maisha au mambo ya maana mwisho wa siku unapoteza mda eti kwasababu unavumilia labda maslahi…My dear moyo auangalii maslahi ktk mapnz au moyo auangalii jina au cheo!Yaani moyo una tabia yakuwa really haswa ukiwa umependa…Usiogope kuonekana unatoka na maskini kwasababu ya macho ya watu hao watu wanaokusema hawana uwezo wa kupambana na moyo wako mpk ukae sawa na upate amani…Kipimo cha amani kinaanza kwako na ww ndio unatengeneza amani yako amani huwezi kuipata kwa mtu yoyote na ndio maana mwisho wa siku tukiforce kupata kwa watu tunaishia kupata MAUMIVU tusiexpect furaha yako anayo fulani Yani usiamini bila fulani huwezi kuwa na amani Ni kweli mda mwingine unaweza ukatengeneza chako lakini kwakuwa Mungu akupanga basi hamfiki popote kwasababu ndo mipango ya Mungu haidhuiliki lkn pia muombe Mungu km unampenda na km hakufai muombe Mungu akufanye uweze kuendelea na maisha mengine kwa usalama bila maumivu au kumfatilia mitandaoni kwa mafekero Yani mdelete moyoni mpk kila sehemu na ukimtanguliza Mungu kila kitu kinaenda sawa tu…Mm nimeamua kuwa na BFF wangu sio kwasababu ya mtu kwasababu moyo umepoa na kupata amani nikiwa nae yeye,Nipo kwenye dunia yangu yani dunia ambayo nishasahau mambo ya kurushana roho na wake wenza,nishasahau kupata presha za mlipuko ukikaa kidogo mara hivi,yaani majanga nimesahau cz ninamtengeneza wangu tena kwa kuufata moyo wangu!Msikubali kufanywa wajinga na wanaume,mtatumika na kupoteza mda kwa watu ambao hawa.

Kwa sasa mrembo huyo yupo katika mahaba mazito kutoka kwa jina Brown, penzi lao lilianza kwa kuita ‘Bff’ katika mitandao ya kijamii.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents