Burudani

WWE: John Cena kufanyiwa upasuaji wa bega

Wakati ambapo WWE ikijiandaa kwa ajili ya Royal Rumble 2016 na WrestleMania 32, mshindi wa mara 15, John Cena atafanyiwa upasuaji wa bega.

960x0

Cena ametangaza hatua hiyo kupitia Twitter, Alhamis hii.

Kumkosa Cena litakuwa pigo kubwa kwa WWE ambayo tayari wachezaji mieleka wake wengi ni majeruhi wakiwemo Daniel Bryan, Sting, Randy Orton, Seth Rollins, Cesaro na wengine.

Hata hivyo wana mieleka wakongwe wakiwemo The Undertaker, The Rock na Brock Lesnar watasaidia kuziba pengo la Cena kama hatoweza kushiriki kwenye WrestleMania 32.

Wachambuzi wa mchezo huo wamedai kuwa ni muda wa WWE kutengeneza staa mwingine huku Roman Reigns akionekana kuwa kipenzi kipya cha wengi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents