Habari

XENOPHOBIA: Wananchi Nigeria waliamsha dude mitaani, Wachoma ofisi za makampuni kutoka Afrika Kusini, Rais wao atoa tamko (+Video)

Wananchi nchini Nigeria wameanza kuandamana na kuvunja ofisi za makampuni yaliyopo nchini mwao yanayomilikiwa na raia wa Afrika Kusini.

Maamuzi hayo yamekuja katika kipindi ambacho, Raia wengi wa Nigeria wanaofanya biashara nchini Afrika Kusini kupigwa na kuchomewa maduka yao na wazawa wa taifa hilo.

Matawi ya makampuni ya Multichoice na MTN nchini Nigeria ni moja ya ofisi ambazo zimeathirika zaidi na maandamano nchini Nigeria.

Ofisi hizo kwa sasa zimefungwa, Licha ya ulinzi mkali uliowekwa na jeshi la polisi nchini humo kuwazuia waandamanaji walioanza jana mchana na leo.

Vurugu za kuwapiga wafanyabiashara wa kigeni nchini Afrika Kusini, Zimeanza wiki moja iliyopita, Na tayari viongozi wa Taifa hilo wametoa onyo kwa wazawa wanaochochea na kufanya vurugu hizo.

Wakati hayo yakijiri, Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari amemtaka Rais wa Afrika Kusini wakae meza moja wajadiliane namna ya kunusuru raia wake wanaoshambuliwa na wazawa nchini Afrika Kusini.

Taarifa hiyo ya Rais Buhari, Imepondwa na Wanaharakati nchini Nigeria wakitaka Rais huyo achukue hatua zaidi ya hapo kwani sio mara ya kwanza ndugu zao kuuawa nchini humo.

Jana Septemba 3, 2019 katika kupinga vurugu hizo, Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa  alitoa kauli yake ya kwanza tangu vurugu hizo zipambe moto, akidai kuwa Serikali yake itajitahidi kulinda mali za raia wa kigeni na kuwachukulia hatua za kisheria watu wote waliokamatwa kwa kujihusisha na vurugu hizo.

Kauli ya Rais Ramaphosa imebezwa na watu wengi mitandaoni, Wakidai kuwa serikali ya Afrika Kusini imeshindwa kuzuia vurugu hizo kwa miaka nenda rudi, Jambo ambalo linahatarisha mahusiano mema na mataifa mengine ya Afrika.

Mpaka sasa watu wanne wameripotiwa kuuawa kwenye vurugu hizo, Na watatu wakiwa ni raia wa Nigeria. Huku watu 50 wakishiliwa na jeshi la polisi kwa kuhusika na vurugu hizo.
https://www.instagram.com/p/B1_XpvZBpS7/

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents