Aisee DSTV!

Yadaiwa huyu ndiye anaekwenda kuchukua nafasi ya Manara Simba, mwenyewe ajitabiria ”Nina Sapraizi kubwa kwenu”

Inakumbukwa kuwa Juni 28 mwaka huu 2019 klabu ya Simba ilitangaza nafasi za kazi katika maeneo kadhaa ambayo ni Office Coordinator/Manager.

Image result for Haji Manara bongo5

Lakini pia ikitangaza nafasi za Digital Platforms Officer ikiwa ni sambamba na Media Officer ambapo ilikuwa mwisho wa kutuma maombi hayo ni 5 July mwaka 2019.

Kutokana na muda huo wa kutuma maombi umeshapita na hivi sasa ni 16 Agosti huwenda nafasi hizo zimeshapata watu na kilichobaki ni kutangazwa.

Kwa taarifa za ndani mpaka sasa zinadai Mtangazaji mahiri kutoka Azam Media, Gift Macha huwenda akachukua nafasi ya Afisa habari wa Simba SC, Haji Manara.

Hii leo majira ya asubuhi, Gift Macha ameandika ujumbe ambao unaongeza wasiwasi ya kile kinachofikiriwa kuwa anakwenda kuchukua nafasi ya Manara ndani ya Simba.

”Unamfahamu huyu jamaa mwenye Tshirt ya Blue? Anaitwa Hassan Bumbuli.. Atakuwa mtu mkubwa pale Yanga hivi karibuni… Huyu mwenye jezi ya Taifa Stars ni mimi.. Nina Sapraizi kubwa kwenu… Hivi karibuni.. Familia ya Kurasa za mwisho.” Ameandika Macha.

https://www.instagram.com/p/B1Nfg4-gGWy/

Ujumbe mwingine ambao unaongeza sitofahamu kwa mtangazaji huyo kutimkia kwa miamba hiyo ya soka ya Msimbazi ni pale alipoandika ujumbe huu.

”Kama wewe si shabiki wa Simba au Yanga, wewe siyo shabiki wa mpira.. Kwa Tanzania lazima upende moja ya timu hizi.. Ni lazima.”

https://www.instagram.com/p/B1HZbAdg9m6/

Image

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW