Habari

Yadaiwa waandamanaji Sudan kuanza kushughulikiwa, Viongozi wa kijeshi wadai wameanza kuwa tishio kwa kueleza sababu hizi

Yadaiwa waandamanaji Sudan kuanza kushughulikiwa, Viongozi wa kijeshi wadai wameanza kuwa tishio kwa kueleza sababu hizi

Viongozi wa kijeshi Sudan wamesema waandamanaji waliopiga kambi mbele ya jengo la wizara ya ulinzi mjini Khartoum wamekuwa kitisho kwa uthabiti wa kitaifa, na kwamba wenye mienendo isiyo mizuri watachukuliwa hatua .

Sudan | Streik (Getty Images/AFP/A. Shazly)

Kwa mujibu wa DW Swahili. Onyo hilo kwa waandamanaji limetolewa na mkuu wa kikosi cha kuingilia kati kuzuia fujo cha RSF, Meja Jenerali Othman Hamed katika taarifa iliyorushwa na vituo vya televisheni, kikiwemo cha televisheni ya taifa. Jenerali huyo amesema gari la kikosi cha kupambana na fujo RSF lilishambuliwa na kutekwa, na akaapa kuwa wahusika wataadabishwa kwa mujibu wa sheria.

”Tunaamini kwamba kambi mbele ya wizara ya ulinzi imekuwa kituo cha uhalifu wa aina zote, na kwamba kambi hizo zimekuwa mahali pasipo salama, ambapo ni kitisho kwa mapinduzi na wanamapinduzi, na kwa uthabiti wa nchi.” Amesema Jenerali Hemed na kuongeza kuwa kwa ushirikiano na vikosi vingine vya usalama wa raia, ”kwa njia za kisheria tutasimamisha vitendo hivyo.”

Waandamanaji waelezea hofu

Sudan Khartum Omer Zainal-Abdin (picture-alliance/Photoshot/M. Khidir)Baraza la kijeshi linakosolewa kutaka kuyateka nyara mapinduzi ya umma wa Sudan

Baada ya kauli hii, waratibu wa maandamano wameelezea hofu yao, kwamba yumkini jeshi likatumia mabavu kuwatawanya waandamanaji. Tarek Abdel Maguid kutoka Vuguvugu kwa ajili ya uhuru na mabadiliko, amesema matamshi kama hayo ya Meja Jenerali Hamed yanadhihirisha malengo halisi ya baraza tawala la kijeshi, ambalo amesema sio mshirika wao katika juhudi za mageuzi.

Baraza la kijeshi la mpito linakajikuta katika mvutano na vuguvugu la waandamanaji wanaolishinikiza kukabidhi madaraka kwa raia, karibu miezi miwili baada ya kuangushwa kwa utawala wa muda mrefu wa rais Omar al-Bashir. Mazungumzo yaliyokuwa yakifanyika baina ya pande hizo kuhusu kuundwa kwa baraza la pamoja la mpito, yamekwama.

Waandamanaji hao wamekataa kubanduka mbele wizara ya ulinzi mjini Khartoum, hati pale pale utawala wa kidemokrasia utakapopatikana.

Mgomo wa siku mbili waambulia patupu

Wimbi jipya la maandamano Alhamisi usiku mjini Khartoum lilianza baada ya mgomo wa siki mbili kumalizika bila kuleta mabadiliko yoyote.

Sudan iko katika eneo la kimkakati, kati ya kanda zinazoyumbishwa na kundi linalojiita Dola la Kiislamu, IS kama Somalia, Misri na Libya, na utangamano wake ni muhimu kwa mataifa yenye nguvu, yakiwemo ya Ghuba ya Uarabu, ambayo yangependa kushawishi mwelekeo wa siasa zake.

Mwandishi wa shirika la habari la Reuters aliyeshuhudia maandamano ya Alhamis jioni, ameripoti kuwasikia waandamaji wakitamka maneno ya kukikashifu kikosi cha uingiliaji kati kuzuia fujo. Hapo jana, baraza tawala la kijeshi liliamuru kufungwa kwa ofisi za shirika la utangazaji la al-Jazeera mjini Khartoum bila kueleza sababu

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents