Burudani ya Michezo Live

Yaelezwa hizi ndio Sababu kubwa za mafuriko katika mataifa ya Afrika mashariki, zikitjwa kuwa ni mbaya zaidi – Video

Yaelezwa hizi ndio Sababu kubwa za mafuriko katika mataifa ya Afrika mashariki, zikitjwa kuwa ni mbaya zaidi

Mvua inayosababisha maafa imewauwa watu 250 na kuwaathiri watu milioni tatu kote Afrika Mashariki katik wiki za hivi karibuni, huku vifo zaidi vikitokea nchini Kenya. Kuharibika kwa nyumba , mazao na barabara zinazosobwa na maji zimetatiza juhudi za utoaji msaadakatika ameneo ya mbali.

Masuala ya Hali ya hewa Darren Bett anaelezea kinachosababisha mafuriko.

Je sio kawaida kuwa na mvua katika kipindi hiki cha mwaka?

Kenya ina mismu miwili ya mvua inayohusishwa na kuvuma kwa pepo za kaskazini na kusini mwa eneo la kusanyiko la pepo za kitropiki (ITCZ). Ni eneo la mvua kubwa na nguruma za radi ambapo pepo za kaskazini mashariki na kusini mashariki hukutana.

Eneo hili lenye hali ya hewa ya unyevunyevu hupita kusini mwa Kenya katika miezi ya Oktoba hadi Disemba na hufahamika kama “mvua fupi”.

Kwa hiyo, hatunabudi kutarajia mvua kunyesha wakati huu wa mwaka nchini Kenya. Lakini hii ni kubwa kuliko ilivyo kawaida.

Lori lililosombwa na amfurikoHaki miliki ya pichaAFP/GETTY
Image captionLori lililosombwa na maji eneo la Isinya takriban kilomita 60 kusini mashariki mwa Nairobi mnamo 15 Machi

Kwa hivyo ni kwanini mvua kubwa inanyesha- je ni ongezoko la joto duniani?

Athari za ongezeko la joto duniani kwa misimu ya jua katika eneo la Afrika Mashariki haziko wazi . Kulingana na hali ya kawaida (na kwa sheria ya fizikia), hali ya hewa ya joto inaweza kuwa na mvuke zaidi wa maji na hivyo inakuwa na uwezekano zaidi wa kuzalisha mvua.

Wataalamu wa hali ya hewa wanasema mvua imeimarishwa na hali ya hewa ya ajabu inayoitwa Indian Ocean Dipole (IOD) ambayo ikiwa katika chanya, inaweza kusababisha kuongezeka kwa viwango vya joto vya majikatika Bahari ya Hindi kwa hadi 2C. Hii husababisha viwango vya mvuke vya juu kwenye maeneo ya Afrika mashariki This leads to higher evaporation rates off the East African coastline and this water then falls inland.

Neno dipole linamaanisha “ncha ” mbili au maeneo mawili yenye utofauti. Ncha mbili za bahari ya Hindi (IOD) hupima tofauti katika viwango vya joto vya sakafu ya baharibaina ya ncha ya magharibi ya Bahari ya Hindi (western pole) na ncha ya mashariki ya bahari ya India kusini mwa Indonesia (eastern pole).

IOD sehemu ya bahari ya Hindi ya eneo linalofahamika kama Pacific El Niño na La Niña.

Sio kawaida kuona joto katika maeneo ya magharibi mwa Bahari ya Hindi lin alosababishwa na chanya IOD. Hii inaisabaisha kuimarika kwa mvua katka maeneo ya Afrika Mashariki na ukame kote Australia.

Ongezeko la joto na unyevunyevu huletwa eneo la bara na pepo zinazorudi karibu na Ikweta, na kuimarisha ITCZ na kusababisha kutokuwepo kwa mawingu zaidi ya gharika.

Maelezo wakati wa mafuriko

Mwaka huu viwango vya joto baharini kati ya magharibi na mashariki mwa Bahari ya Hindi vimerekodiwa kuwa ni vya kuvunja rekodi na mvua katika baadhi ya maeneo ya kenya imekuwa ya juu zaidi ya kawaida.

Uhusiano kati ya IOD na mabadiliko ya tabi nchi na vipindi vya mvua ni masual aya kufanyiwa utafiti zaidi, kwasababu eneo la IOD yenyewe lilitambuliwa 1999.

Je Kuna mvua zaidi siku zijazo?

Athari za mvua kubwa Afrika Mashariki

Kwa kipindi kifupi , eneo la upembe wa Afrika linatarajiwa kuwa na mvua zaidi huku pepo za kitropiki zitakapokua zinafika kutoka Bahari ya Hindi.

Katika msimu Disema, mvua inatarajiwa kuendelea katika maeneo ya Kusini magharibi mwa Kenya, Tanzania, Malawi na Kaskazini mwa Zambia.

Licha ya kwamba IOD chanya inatarajiwa kupoungua, kwasababu utofauti wa viwango vya joto umevunja rekodi , mvua inatarajiwa kuwa kubwa kuliko kawaida

Viwango vya unyevu wa ardhi ni vya hali ya juukwa hiyo kiwango kidogo cha mvua kitakua na athari.

Bado kutakuw ana mvua mwezi januari na Februari , kipindi kijacho cha mvua ni Machi hadi Mei.

Kipindi hiki hufahamika kama “kipindi kirefu cha mvua” wakati ambapo mvua kawaida huwa kubwa kuliko wakati wa “kipindi kifupi cha mvua”.

Historia imetuonyesha kuwa mvua hainyeshi katika kipindi kirefu kila mwaka.

Mwaka 2016 na 017 kipindi chha “mvua ya muda mrefu” katika maeneo ya Afrika haikunyesha na kusababisha maeneo ya Kenya kuwa na mzozo wa chakula, wanyama kufa kutokana na njaa na kunyauka kwa mimea kutokana na ukame.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW