Fahamu

Yaelezwa huyu ndio mwanamke aliyepigwa busu mara nyingi zaidi duniani

Wakati fulani katika karne ya 19, mwili wa msichana mdogo ambaye alikuwa amekufa maji uliokolewa katika mto Seine.

Kama ulivyokuwa utamaduni wakati huo, mwili wake ulikuwa wazi katika chumba cha kuhifadhia maiti cha mjini Paris, kukiwa na matumaini kwamba huenda mtu anaweza kuuona na kumtambua, lakini hakuna aliyemtambua.

Katika picha hii ya maelezo iliopigwa mwaka 1816, watu wanaonekana wakitembelea chumba cha wafu wakitazama miili , kitu kilichopendelewa sana wakati huo.

Daktari wa upasuaji aliyekuwa katika zamu alivutiwa na tabasamu ya uso wa msichana huyo hatua iliomfanya kumuomba mtengenezaji mask au barakoa kuunda uso kama wake.

Ni kutokana na hatua hiyo ndiposa uso huo wa mwanamke aliyefariki ulihifadhiwa milele.

Uso kuhifadhiwa

Baadaye, mask hiyo ilianza kuonekana ikiuzwa huku uso huo wa msichana huyo mdogo ukionekana kama unaowapatia msukumo wasanii, washairi na waandishi wa riwaya, wote wakijaribu kubuni hadithi kuhusu mwanamke huyo waliyemtaja kuwa Mona Lisa aliyekufa maji.

Miaka mingi mshairi kutoka Austria na mwandishi wa riwaya Rainer Maria Rilke, raia Mfaransa Louis Aragon, msanii wa Marekani Man Ray na mwandishi wa riwaya wa Urusi Vladimir Nabokov wote walivutiwa na mask hiyo na kuna kipindi fulani hakuna saluni iliokosa mask hiyo katika ukuta wake Ulaya.

Mojawapo ya hadithi za kwanza ambapo mask hiyo ilionekana ni ile ya riwaya ya 1899 Kwa jina ‘The worshiper of the image’ ilioandikwa na Richard le Galliene, ambayo inaelezea jinsi mask hiyo ‘inavyomroga’ na kumuharibu mshairi mchanga.

Gente de visita en la morgue de París para ver cadáveres, en esta ilustración de R.B. Peake de 1816.

Wengi wao wanaelezea hadithi hiyo ya msichana asiye na hatia anayewasili mjini Paris kutoka mashambani , anatongozwa na mtu tajiri na kuwachwa anaposhika ujauzito wake . Baada ya kukosa mtu wa kumsaidia , anajirusha katika mto Seine.

Lakini kuna hadithi nyengine.

Ni kufa maji kwa aina nyengine – ama tukio la kufa maji lililosaidia jina la msichana huyo kuingia katika historia ya tiba duniani.

Mwaka 1955 raia wa Norway kwa jina Asmund Laerdal aliokoa maisha ya mwanawe wa kiume , Tore kwa kuuopoa mwili wake katika maji kwa wakati na kuweka wazi njia zake za kupumua mwilini.

Wakati huo, Laerdal alikuwa muundaji wa wanasesere, kama vile doli na magari kutokana na plastiki laini.

Alipotakiwa kutengeneza kifaa cha kufunza watu mbinu mpya ya kuwafufua inayoshirikisha kumfinya kifua na ‘kumpiga busu’ hatua inayoweza kuokoa moyo wa mwanadamu ambao ulikuwa umewacha kupiga.

Uzoefu alioupata na mwanawe wa kiume miaka kadhaa iliopita ulimfanya kukubali.

Bustos de La Desconocida del Sena en el taller Lorenzi de París.

Aliamua kuunda mwanasesere aliyekosa fahamu ambaye alikuwa anahitaji CPR ili kukufuka. Laerdal alimtaka mwanaseser wake kuwa asili.

Na aliona kwamba mwanasesere wa kike hatawaogofya wale watakaokuwa wakifunzwa kufufua mwanadamu CPR (cardiopulmonary resuscitation). Alikumbuka mask iliokuwa imetundikwa ukutani katika nyumba ya bibi yake, hivyobasi akaamua kwamba uso wa musk hiyo ndio utakaotumika katika mafunzo hayo.

Hivyobasi iwapo wewe ni miongoni mwa watu milioni 300 waliofunzwa CPR umefanikiwa kuweka madomo yako katika mdomo wa mask hiyo ya msichana.

Hio ndio sababu anaitwa mwanamke aliyepigwa busu mara nyingi zaidi duniani.

Chanzo BBC

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents