Afya

Yaelezwa kutopiga mswaki huathiri Ubongo, fahamu zaidi

Tunapokutana na wagonjwa wa moyo , Alzheimer au ugonjwa wa kisukari hatufikirii kwamba hawajapiga mswaki vizuri. Tunahusisha uchafu wa kinywa na matatizo ya mdomo kama vile vidonda, kuvimba kwa ufizi na harufu mbaya, lakini sio na matatizo yanayosababishwa na viungo vingine vya mwili.

Ukweli ni kwamba harufu nzuri ya kinywa ni muhimu katika utendakazi mzuri wa mwili.

Magonjwa ya kinywani yanaweza kuchangia magonjwa mengine.

Kuna ushahidi kwamba bakteria walio mdomoni wanaweza kusambaa hadi katika maeneo mengine ya mwili na kusababisha matatizo.

Hata katika ubongo wetu!

Njia ya pekee ya kuzuia matatizo ya kinywa ni kuimarisha usafi wa mdomo wako
Njia ya pekee ya kuzuia matatizo ya kinywa ni kuimarisha usafi wa mdomo wako

Kwa jumla , kila mtu ana kati ya spishi 100 na 200 za bakteria wa kinywani kati ya spishi 700 zinazotambulika.

Tunapomuuliza mtu ni bakteria wangapi waliopo ndani ya mate ya mililita moja , wengi hupuuza jibu lake .Kuna bakteria takriban milioni 100 katika mililita moja ya mate.

Bakteria hawa huishi katika meno, ulimi, ufizi na maeneo mengine ya kinywa. Ukijumlisha bakteria wote walio mdomoni , idadi yao hufikia bilioni kadhaa.

Mbali na tabasamu inayovutia, afya ya mdomo ni muhimu kwa fya yote ya mwili wako
Mbali na tabasamu inayovutia, afya ya mdomo ni muhimu kwa fya yote ya mwili wako

Kwa jumla ni kwamba viumbe hawa wadogo watakuwa marafiki wetu tunapowalinda. Kwanza hutulinda dhidi ya viini vinavyosababisha magonjwa.

Athari chanya

Wakati bakteria wapya wanapoingia mdomoni , ni vigumu kwao kuweza kuishi, kuna jeshi la bakteria wanaoishi katika eneo hilo.

Ukiongezea, viumbe hao walio na faida kwa mwili wa mwandamu hubadilisha madini ya nitrate kutoka katika mboga na matunda hadi kuwa nitrite.

Haya yanaweza kuwa na athari chanya katika mwili kama vile kupunguza shinikizo la damu mbali na kukabiliana na kisukari.

Kwa kawaida , bakteria wetu sio hatari, lakini wanaweza kusababisha magonjwa ya kinywani miongoni mwa watu kutokana na uchafu.

Chakula kisicho na afya ama uchafu wa mdomoni unaweza kusababisha ukosefu wa usawa wa bakteria mdomoni. Baadhi ya bakteria huongezeka kwa idadi huku wengine wakipungua.

Baadhi ya bakteria hupungua na wengine kuongezeka na hivyobasi kusababisha ukosefu wa usawa
Baadhi ya bakteria hupungua na wengine kuongezeka na hivyobasi kusababisha ukosefu wa usawa

Kwa mfano , iwapo tunatumia sukari , bakteria wanaoishi katika mashimo ya meno huongezeka. Bakteria hao hubadilisha sukari na kuwa asidi ya kaboni. Baadhi ya bakteria wanaozalisha asidi hiyo hujizatiti na kuishi huku wengine wakifariki. Tunapotumia sukari kwa wingi , bakteria wanaokula sukari na kuzalishi asidi ya kaboni huongezeka katika mashimo ya meno suala linaloharibu jino.

Baada ya muda hii inaweza kusababisha kuoza kwa jino.

bakteria kutoka katika jino linalooza zinaweza kusambaa hadi sehemu nynegine za mwili na kusababisha matatizo ya kiafya
bakteria kutoka katika jino linalooza zinaweza kusambaa hadi sehemu nynegine za mwili na kusababisha matatizo ya kiafya

Magonjwa mengine

Kuna ushahidi kwamba magonjwa ya kinywani yanaweza kuchangia matatizo tofauti .

Mtu anapokuwa na tatizo la kinywani huongeza hatari , kwa mfano ugonjwa wa rheumatoid arologist, atherosulinosis, shinikizo la damu, ugonjwa wa Alzheimers, ugonjwa wa sukari, na matatizo wakati wa kujifungua.

Watu wanaougua matatizo ya kinywani , huwa na sababu tofauti zinazoweza kusababisha magonjwa mengine.

Kwa mfano, idadi kuu ya molekyuli zinazozalishwa na seli za binadamu na kusababisha uvimbe katika ufizi zinaweza kufikia viungo vingine vya mwili na kusababisha arhari katika maeneo hayo. Kumtembelea daktari wa meno ili kutibu matatizo hayo ya kinywa ni muhimu.

Hivi majuzi kundi moja la watafiti lilifanyia utafiti ubongo wa watu waliofariki kutokana na AlZheimer. Waligundua chembechembe za DNA kutoka kwa Porhyromonas gingivalis na Enzymes inayoitwa gingipain, ambayo inavunja protini za binadamu. Zaidi ni kwamba idadi ya enzymes hizo zilitokana na athari zinazotokana na ugonjwa huo.

Watafiti hao waliwapatia panya idadi kubwa ya bakteria hao na viini hivyo vikaathiri ubongo wao.Wanyama hao walianza kuwa na dalili za ugonjwa wa Alzheimer, lakini wale waliopatiwa tiba ya gingipain waliimarika kiafya.Hitimisho moja ni kwamba Porhyromonas gingivalis inaweza kufikia ubongo na, kwa miaka mingi, inachangia ukuaji wa Alzheimer’s.

Kila kitu huanza na kuoza kwa jino
Kila kitu huanza na kuoza kwa jino

Afya ya binadamu ina uhusiano mzuri wa viumbe vinavyoishi ndani yake ikiwemo vile vilivyo ndani ya mdomo.Kutokana na ukosefu wa usafi ama mlo usio na Afya , bakteria wanaweza kusababisha matatizo mdomoni na maeneo mingine ya mwili.

Kupiga mswaki mara mbili kwa siku.

Muungano wa madaktari wa meno nchini Marekani unapendekeza kupiga mswaki mara mbili kwa siku kwa kutumia dawa ya meno na kumtembelea daktari wa meno mara kwa mara.Magonjwa ya kinywa hayafai kuwachwa bila tiba. Mbali na kuonyesha tabasamu nzuri , ni muhimu kuimarisha afya ya mwili wako wote.

Chanzo BBC.

https://www.youtube.com/watch?v=P7uvoKOYq5I

https://www.youtube.com/watch?v=Z7RtbEf6ibA

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents