Habari

Yaelezwa matapeli nchini Kenya, wawasababishia zaidi ya waislam 29 kukosa Hijja Mecca

Yaelezwa matapeli nchini Kenya wawasababishia zaidi ya waislam 29 kukosa Hijja Mecca

Takriban Waislamu 30 nchini Kenya wanadaiwa kushindwa kusafiri kwenda Mecca nchini Saudi Arabia kwa ajili ya kutekeleza nguzo muhimu katika dini ya kiislam ya Hija baada ya kutapeliwa na wakala wa Hajj nchini Kenya. Wanaodaiwa kutapeliwa wengi wao ni wazee ambao walikuwa wakijiandaa kwa ajili ya kushiriki ibada ya hija inayotekelezwa na waumini wa kiislamu kila mwaka mjini Makka Saudi Arabia.

Wakala huyo anadaiwa kukusanya kati ya dola 3500 na 4000 kutoka kwa kila mmoja wa waumini hao na ”kutoweka”

Omar Said Hassan ni mmoja wa watu 30 wanaodaiwa kutapeliwa na mwanamume huyo aliyewahakikishia kuwa kampuni yake ingewasaidia na mipango yote ya kusafiri kwa hija mwaka huu:” Wiki iliyopita nilikutana na ajenti ambao wanafaa wapeleke watu Hijja.

Bwana Omar anasema hawezi tena kushiriki ibada ya Hija baada ya muda wa kusafiri kuisha na amepoteza pesa za paspoti anazodai zimechukuliwa na wakala wa Hajj
Image captionBwana Omar anasema hawezi tena kushiriki ibada ya Hija baada ya muda wa kusafiri kuisha na amepoteza pesa za paspoti anazodai zimechukuliwa na wakala wa Hajj

Mimi nimelipa dola 2,500 na mke wangu amelipa 2,700 tulikuwa tunategemea kwenda hijja na tunasikia jamaa huyu amekwepa tayari alikuwa na paspoti zetu na si peke yangu tulikuwa na watu 28 wengine” na kuongeza kuwa wakala huyo wa kampuni inayofahamika kama Itihaf tayari anasakwa na polisi nchini Kenya.

Kwa mujibu wa BBC.Taarifa zinasema kuwa polisi wamevamia chumba cha hoteli katika kitongoji cha Eastleigh, mjini Nairobi ambapo waligundua baadhi ya pasipoti ambazo hazikuwa na visa ndani yake.

Hijja inaanza Ijumaa tarehe 9 Agosti 2018

‘Tunatarajia polisi wafuatilie suala la jamaa huyu…apatikane, ndio maana tulimripoti polisi” amesema Bwana Omar ambaye alitarajia ”kumpeleka mke wake Makka kuhijji kwa mara ya kwanza”.

Bwana Omar anasema muda wa kwenda Hijja kwa sasa umekwisha na hawezi tena kwa sasa kwenda kutokana na kwamba pesa aliyokuwa ameipangia safari hiyo, imepotea.

Hassan Omar anatoa wito kwa Waislamu wenzake wanaopanga kwenda kuhijji kwa kuwatumia mawakala, wathibitishe kwanza iwapo ni wakala halali, ili wasipoteze pasipoti na pesa zao. ”Watafute maajenti wanaofahamika”, anasema

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents