Aisee DSTV!
SwahiliFix

Yaelezwa Pundamilia wa ajabu, aliyepatikana Kenya amehamia Tanzania, Fahamu zaidi

Yaelezwa Pundamilia wa ajabu, aliyepatikana Kenya amehamia Tanzania, Fahamu zaidi

Pundamilia wa ajabu ambaye hivi karibuni alionekana katika mbuga ya wanyama ya Mara nchini Kenya amevuka mpaka na kuingia ndani ya Mbuga ya Wanyama ya Taifa ya Serengeti pamoja na pundamilia wengine waliokuwa wanahama pamoja na Nyumbu , limeripoti gazeti la Nation nchini Kenya

Kinyume na pundamilia wengine wenye mistari kwenye ngozi yake pundamilia huyo anamadoadoa meupe na mistari michache myeupe inayofifia mwilini mwake, jambo lililomfanya kuwa ni wa kipekee.

Taarifa ya kuhamia kwake nchini Tanzania imethibitishwa na makumi ya watalii na walinzi wa mbuga za wanyama pamoja na katibu wa shirika la madereva wa magari ya utalii nchini Kenya Felix Migoya ambaye amesema kuwa punzamilia huyo mchanga mwenye umri wa mwezi mmoja hivi , kwa sasa yuko katika eneo la kaskazini mwa mbuga ya wanyama ya Serengeti Serengeti.

Alipinga taarifa za uvumi kwamba kivutio hicho kipya cha utalii katika mbuga ya wanyama ya Mara kilikamatwa na kufungiwa kuhifadhiwa mahali pake kama ilivyoelezwa katika mitandao ya habari ya kijamii katika kipindi cha wiki tatu zilizopota, Limeripoti gazeti la Daily Nation nchini humo.

“Taarifa za mitandao ya kijamii ni feki , pundamilia anayeonyeshwa kwenye mitandao ya kijamii ni mkubwa na alikamatwa nchini Afrika Kusini katika tarehe ambayo haijulikani mika kadhaa iliyopita ,”alisema Bwana Migoya alipozungumza na gazeti la the Nation Jumatano.

Wazazi wa pundamilia huyo mchanga wako katika kipindi cha mwaka cha kuhama kwa zaidi ya mamilioni ya wildebeest baina ya mbuga ya wanyama ya Serengeti na hifadhi ya wanyama ya Maasai Mara – tukio ambalo huwavutia watalii kutoka maeneo mbali mbali duniani.

PundamiliaHaki miliki ya pichaNATION MEDIA GROUP

Tukio hilo, ambalo liliwekwa katika orodha ya ”Maajabu Saba ya Dunia ‘, kwa kawaida kuanza katikati ya mwezi Juni hadi mwezi Oktoba.

Katika kipindi hiki, nyumbu hukutana kabla ya kufanya safari yao ya kurejea sambamba na mamia ya pundamilia , swala na wanyama wengine wanaotafuta malisho.

Pundamilia huyu wa ajabu mweusi kwa mara ya kwanza aligunduliwa na kupigwa picha mapema mwezi Septemba karibu na mto Mara River na Antony Tira, mwongozaji maarufu wa safari za watalii kutoka kabila la Maasai na alimpiga picha hiyo katika kambi ya utalii ya Matira Bush iliyopo ndani ya mbuga ya wanyama.

Bwana Tira alimuita pundamilia huyo mchanga jina la baba yake ‘Tira’.

Si mweusi kabisa , na kutokana na utofauti wa ngozi yake katika sehemu mbali mbali za mwili wake: “Kutokana na rangi yake , pundamilia huyo amekuwa maarufu ghafla na amekuwa kivutio cha watalii katika mbuga ya Mara na sasa huenda watalii wakaelekea Serengeti kwani watu wengi wanamfuata kiumbe huyo wa ajabu ,” aliongeza Bwana Migoya.

Tangu mpigapicha Tira alipotuma picha ya pundamilia huyo na kuwaalika watu kuja kumuona, watu wengi wamekuwa wakiongezeka katika hifadhi ya wanyama ya Mara na kusababisha ‘msongamano ‘ mkubwa wa watukatika hifadhi hiyo..

Chanzo BBC

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW