Habari

Yaelezwa takribani raia wa kigeni 600, wamekamatwa na polisi Afrika Kusini wakihusishwa na uhalifu – Video

Yaelezwa takribani raia wa kigeni 600, wamekamatwa na polisi Afrika Kusini wakihusishwa na uhalifu

Takribani raia wa kigeni 600 wamekamatwa na polisi Afrika Kusini wakituhumiwa kujihusisha na uhalifu. Operesheni maalumu dhidi ya uhalifu imeendeshwa katika jiji kuu la kiuchumi la Johannesburg, lakini wapo ambao wanahofu operesheni hiyo kuzaa mashambulizi ya chuki dhidi ya wageni. Mashambulizi ya chuki dhidi ya wageni nchini Afrika Kusini yanachochewa na mdororo wa kiuchumi na ukosefu wa ajira kwa wenyeji.

Polisi wanadai kuwa “shehena kubwa” ya bidhaa bandia na silaha za moto katika majengo mbali mbali.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter kiongozi mkuu wa jimbo la Gauteng, David Makhura amesema operesheni hiyo ni sehemu ya kulifanyia usafi jimbo.

“Tuansafisha kati kati ya jiji letu. Hatutapumzika mpaka tulirejeshe jiji mikononi mwetu. Tunatuma ujumbe mkali kwa wote ambao wanahisi wanaweza kuishi kwenye majengo yetu kinyume na sheria,” ameandika Makhura kwenye mtandao wa Twitter.

Katika ujumbe mwengine, alisukuma lawama moja kwa moja kwa wageni. “Baadhi ya raia wa kigeni ambao wanauza bidhaa bandia na kukaa kwenye majengo yetu kinyume cha sheria wamewashambulia askari wetu kwa chupa na mabomu ya petroli. Shambulio hili haliwezi kuvumilika, tutajibu kwa nguvu ya dola kulinda utawala wa sheria.”

Kwa mujibu wa BBC.Kauli hiyo hata hivyo imepingwa na baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii ambao wanaonya kuwa inaweza kuchochea mashambulizi ya chuki dhidi ya raia wa kigeni.

“Umefikiaje hitimisho kuwa ni raia wa kigeni tu ndio ambao wameshiriki (katika ghasia)?” ameuliza Bw Baba Ka Thando.

“Je, kwani ni muhimu kujua jinai imetendwa na mwenyeji au mgeni? Jinai ni jinai, shughulikia wahalifu lakini usichochee mashambulizi ya chuki,” ameeleza Dr J. Tsedudzayi pia kupitia mtandao wa Twitter.

Mashambulizi ya chuki dhidi ya wageni nchini Afrika Kusini yamekuwa yakitokea mara kwa mara.

Wenyeji, hususani vijana wamekuwa wakiwashambulia wageni kwa tuhuma za kufanya uhalifu na kuwapoka nafasi za ajira nchini mwao.

Mashambulizi hayo kwa kingereza hufahamika kama xenophobia.

Mwezi machi mwaka huu watu watatu waliuawa katika jiji la Durban huku waandamanaji wakilenga maduka ya ya wageni.

Mwaka 2008 wimbi baya zaidi la mashmbulizi hayo lilifanyika na watu takribani 60 waliuawa. Mwaka 2015 wakauawa saba.

Mwezi Februari mwaka jana, mwanafunzi wa shahada ya uzamivu katika Chuo Kikuu cha Johannesburg kutoka Tanzania Bw Baraka Leonard Naferi aliuawa katika shambulio linalodhaniwa kuwa ni la chuki.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents