Habari

Yafahamu Majiji 20 yanayoongoza kwa kuwa na Mabilionea wengi zaidi duniani

Ufahamu mji wako upo nambari ngapi

Kwa mujibu wa sensa ya hivi karibuni ya kuhusu hali ya utajiri na matajiri duniani iliyofanywa na shirika la kimataifa la uchumi linalo fahamika kama Wealth X lenye makao makuu yake sehemu mbili ambazo ni New York Marekani pamoja na London nchini Uingereza, Limelitaja jiji la New York kutoka Marekani, kuwa kwasasa jiji hilo ndio linaloongoza kwa kuwa na Mabilionea wengi zaidi kuliko miji mingine yote duniani.

Likifuatiwa na jiji la Hong Kong la nchini China,Kama unaishi Hong Kong, Hong Kong ilipata mabilonea zaidi ya 20 mwaka 2017, huenda umeshawahi kumsikia Li Ka-shing. Na pengine kumpatia pesa. Mfanyabiashara huyo wa miaka 90 ni mtu wa 23 tajiri zaidi duniani. Thamani ya mali zake kwa jumla inakadiriwa kuwa dola bilioni 37.7 Ka-shing amewekeza katika biashara tofauti kuanzia sekta uchukuzi hadi za kifedha, kawi na kampuni za kutoa huduma.

Bilionea huyu ni mfano tu wa utajiri unaopatikana katika eneo hilo linalotaka kujitenga na China,  Hong Kong sasa ina jumla ya mabilionea 93, idadi ambayo imeongezeka kwa 21 zaidi kutoka mwaka 2016. Sensa hiyo pia imebaini kua nusu ya miji 10 iliyo na idadi kubwa ya mabilionea iko katika mataifa yanayoendelea katika maeneo yanayotajwa kuwa na viwango vya juu vya ukosefu wa usawa duniani.

Kuongezeka kwa “mabilionea wanaoibuka” pia kumechangia kuibuka kwa idadi ya maeneo ya bora zaidi ya kuekeza duniani. Sensa hiyo ilirekodi watu 2,754 ambao walikua na mali ya thamani ya dola bilioni 1 au zaidi mwaka 2017. Mali yao kwa pamoja ikijumlishwa ni takriban dola trilioni 9.2 -hii ikiwa ni zaidi ya pato jumla ya mataifa ya Ujerumai na Japan ikijumlishwa pamoja.

Miji iliyo na mabilionea wengi duniani (kwa mujibu wa: Wealth-X)
Mji Idadi ya mabilionea mwaka 2017 Mabadiliko tangu mwaka 2016
1. New York 103 +1
2. Hong Kong 93 +21
3. San Francisco 74 +14
4. Moscow 69 -2
5. London 62 0
6. Beijing 57 +19
7. Singapore 44 +7
8. Dubai 40 +3
9. Mumbai 39 +10
9. Shenzen (China) 39 +16
11. Los Angeles 38 +6
12. Istanbul 36 +8
13. Sao Paulo 33 +4
14. Hangzhou (China) 32 +11
15. Tokyo 30 +8
16. Paris 29 0
17. Riyadh 26 +2
18. Jeddah 23 +1
19. Shanghai 23 +3
20. Mexico City 21 +2

Kuongezeka kwa idadi ya mabilionea kumezua maoni kinzani miongoni mwa wataalam juu ya madhara yake ya kijamii. Kambi moja inaangazia masuala ya kimaadili yanayotokana na kupanuka kwa pengo la mapato katika jamii. Suala hilo limeangaziwa pia katika ripoti ya kila mwaka ya shirika la Oxfarm ambayo inapendekeza watu matajiri zaidi watozwe kodi kubwa ya juu. Kambi nyingine inawachukulia mabilionea kama chachu ya maendeleo katika jamii.

Mfanyibiashara Mukesh Ambani, mtu tajiri zaidi nchini India, anaishi kwa nyumba ya ghorofa 27 katika mji wa Mumbai, ambao nusu ya watu wanaishi katika mitaa ya mabanda.

Mwaka 2016, mwanauchumi wa benki ya dunia Caroline Freund alitetea maoni yake katika vitabu vyake vinavyofahamika kama Rich People, Poor Countries: The Rise of Emerging-Market Tycoons na Their Mega Firms. Bi Freund aliambia BBC kuwa “Kuna mwenendo wa kuwakosoa watu matajiri lakini watu hawa si sawa. Mali inaweza kukuzwa kwa njia tofauti, kwa hivyo manufaa yake kwa jamii inategemea zaida mfumo wa mali yenyewe,”.

Jarida la Forbes la Marekani linasema kuwa sasa mabilionea wamesambaa katika mataifa mataifa tofauti duniani. China, India na Hong Kong zimeandikisha ukuaji wa mara mbili ya idadi ya mabilionea wao. Mataifa hayo yaliongeza idadi ya mabilionea barani Asia hadi watu 784, amabo walishinda idadi ya mabilionia America Kaskazini (727) kwa mara ya kwanza katika historia.

Katika maeneo ya bara nchini China, 1% ya watu matajiri wanamiliki thuluthi tatu ta utajiri wa nchi hiyo mwaka 2016, hayo ni kwa mujibu wa utafiti wa chuo kikuu cha Beijing. Afrika, bara ambalo linajaza nafasi 19 kati ya 20 za mwisho kwenye orodha ya Maendeleo ya Binadamu Duniani, sasa ina mabilionea 44 – ambao wana mali ya jumla ya thamani ya $93 bilioni.

Mataifa 10 yaliyo na mabilionea (kwa mujibu wa Wealth-X)
Nchi Idadi ya mabillionea Mabadiliko (%) 2016-17 Jumla ya mali ($ billion)
Marekani 680 9.7% 3,167
China 338 35.7% 1,080
Ujarumani 152 17.8% 466
India 104 22.4% 299
Uswizi 99 15.1% 265
Urusi 96 -4.0% 351
Hong Kong 93 29.2% 315
Uingereza 90 -4.3% 251
Saudi Arabia 62 8.8% 169
Muungano wa milki za Kiarabu(UAE) 62 19.2% 168

Kinadharia, watu hawa wakibuni taifa lao, litakuwa taifa la nane lililo na kiwango cha juu cha pato jumla la taifa miongoni mwa mataifa mwa mataifa 54 ya Afrika. Ni sehemu chache zimeshuhudia ongezeko la haraka la idadi ya watu matajiri zaidi kuliko India.

Katikati ya miaka ya tisini , ni wahindi wawili tu walishitikishwa katika orodha ya Forbes ya watu matajiri na mashuhuri. Kufikia mwaka 2016, India ilikua na maombi 84. Data ya mwaka 2016 ya Benki ya Dunia inakadiria kuwa raia milioni 280 walikua masikini zaidi nchini India.

Utafiti wa uchumi unaonyesha kwamba makampuni yaliyoanzishwa katika masoko yaliyoibuka na wajasiriamali huajiri watu wengi zaidi. Karibu wafanyikazi 80,000 katika kampuni hizo, huchangia pakubwa bishara zinazomilikiwa na mabilionea waliyorithi mali au kununua mali ya umma.

Makampuni ya ushauri McKinsey inatabiri kuwa kufikia mwaka 2025 masoko ya yanayoibuka yanapaswa kuwa na 45% ya kampuni 500 ambayo nusu yake inamilikiwa na mabilionea duniani.

Oxfam, hata hivyo ina takwimu tofauti ambayo imezua mjadala: kwa mujibu wa wataalamu wa mashirika yasiyokua ya kiserikali, kuongezeka kwa kiwango cha ukosefu wa usawa kati ya mwaka 1990-2010 kumesaidia mamilioni ya watu kote duniani kujipusha umasikini licha ya kupungua kwa viwango vya umasikini katika miaka hiyo 20.

Rebecca Gowland, Mkuu wa kitengo cha usawa wa shirika la Oxfarm ameimbia BBC kuwa “Mara nyingi, ukuaji mkubwa katika uchumi wa masoko yanayo ibuka umeongeza faida ya benki ya watu wenye utajiri, huku ukuaji huo ukiwa hauna manufaa yenya tija kusaidia kwa watu maskini zaidi katika jamii”.

Bi Gowland, pia anasema nchi kama Nigeria ambayo inajivunia ukuaji imara na kuwa na mtu tajiri zaidi barani Afrika, umasikini umeongezeka”.

Katika utafiti wao wa mwaka 2015, msomi wa Marekani Sutirtha Bagchi kutoka chuo kikuu cha Villanova na Jan Svejnar wa chuo kikuu cha Columbia walihoji kuwa viwango vya ukosefu wa usawa havihusiani kwa vyoyote na sababu ya ni kwa nini hakuna usawa katika jamii.

Utafiti huo uliyohusisha mabilionea kutoka mataifa 23 mwaka 1987-2002, ulibaini kuwa mabillionea wanapopata mali yao kutokana na uhusiano wa kisiasa, mali hiyo huwa na athari kwa uchumi.

Mali iliyo mikononi mwa watu wachache huchangia kubuniwa kwa sera kali kutokana na muingilio wa serikali, ambayo haina manufa makubwa kwa jamii.

Swala jingine tata katika mdahalo unaozunguka mabilionea duniani ni lile la kurithi mali.

Wataalamu kama mwanauchumi wa Ufaransa Thomas Piketty, anasema hali hiyo inarudisha nyuma ukuaji wa kijamii, kwa sababu matajiri huwapokeza mali watoto wao. Japo sensa ya kampuni ya Wealth X imegundua kuwa wengi wa watu wenye utajiri wanaweza kuorodheshwa kama watu waliyojijenga wenyewe mwaka 2017 kwa 56.8%, kiwango cha mali iliyotokana na urithi kiliongezeka mwaka 2017 kwa 13.2%, kutoka 11.7% mwaka 2016.

Chanzo BBC

By Ally Juma.

Chanzo BBC

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents