Habari

Yafahamu Majiji matano masikini zaidi Duniani

Yafahamu Majiji matano masikini zaidi Duniani

Licha ya maendelea kuzidi kuongezeka katika baadhi ya nchi pamoja na miji mbalimbali katika maeneo husika lakini kumeendelea kuwa na changamoto kubwa sana katika baadhi ya miji hapa duniani kuweza kupata maendelea kwa haraka kutokana na ukuaji wa Sayansi na Teknolojia.

Maendelea katika sehemu yeyote huchangiwa na vitu mbalimbali mfano miundombinu, pamoja na watu husika. Miundo mbinu hiyo mfano Barabara,maji,umeme,shule,hospitali na huduma zote za kijamii.

Kwa upande mwingine Serikali zinamchango mkubwa sana katika kuhakikisha inatengeneza miundo mbinu bora ili kuweza kusababisha chachu ya maendeleo katika nchi husika hata katika miji husika ikisaidiana na wadau au makampuni binafsi.

Lakini biashara ndio imepelekea kuwa chachu kubwa sana ya maendelea katika maeneo mbali mbali ingawa sekta zote zinahusika katika kuleta maendeleo ila biashara ndio kinara wa sekta inayosababisha maendelea kutokana na kodi zinazotozwa kutoka kwa wafanya biashara na hata makampuni mbalimbali yanayofanya biashara.

Maendelea katika sehemu yeyote huletwa na watu husika katika maeneo husika wakisaidiana vyema na serikali pamoja na wadau mbalimbali. Kutokana na utafiti uliofanywa na ” We are the top ten” umeonesha kuwa Majiji yafuatayo ndio yanayoongoza kwa umasikini zaidi Duniani kutokana na sababu mbalimbali zinazopatikana katika maeneo hayo.

1. Monrovia. Liberia

Huu ni mji mkuu wa Liberia,hili ndio jiji taabani zaidi duniani mgao wa umeme katika jiji hilo umechangia kwa kiasi kikubwa kurudisha nyuma maendeleo katika jiji hilo,hasa katika uzalishaji wa Saruji,Uchimbaji wa Mafuta na uzalishaji wa chakula na inasemekana nyumba nyingi katika mji huo hazina Umeme. huku pia tatizo la maji safi likionekana kuwa ni kikwazo kwani watu wananunua maji kupitia kwenye madumu ambayo hutokana na watu waliyohifadhi kwenye matenki,huku suala la kiafya likiwa ndio tabu sana

2.CONAKRY, GUINEA.

Jiji hili linapaswa kuwa na watu takribani milioni mbili,hili ndio jiji ambalo huduma za mawasiliano ni shida sana,kwani uchumi wake unategemea sana katika kuhifadhi na kusafirisha mizigo ya ndizi pamoja na unga wa Aluminium  pia kukiwa na viwanda vidogo vinavyotengeneza bidhaa za chakula pamoja na ujenzi,huku ukosekanaji wa maji na umeme vikiwa ni vyanzo vikubwa vya kudumaza uchumi wa jiji hilo.

3.ANTANANARIVO, MADAGASCAR.

Jiji hili ndi kitovu kikubwa cha kisiasa, kiuchumi, elimu na kitamaduni katika taifa hilo la Madagasca,lakini hapa ndipo yalipo makao makuu ya nchini sehemu anakoishi rais wa Madagasca,bunge,baraza la seneta pamoja na mahakama ya nchi hiyo,huku sekta ya kilimo ikiwa ndio chachu ya maendeleo katika jiji hilo ambako hulima na kufuga na wanasema katika jiji hilo huwezi kumiliki ardhi kisheria vinginevyo utaruhusiwa kuikodisha au kununua nyumba pekee,ingawa ardhi kubwa imechukuliwa kinyume na sheria.Pia jiji hili ndio linalotajwa kuwa na huduma mbovu za vyoo kwa wakazi wake,lakini suala la usafi likiwa ni tatizo kubwa katika jiji hilo huku barabara zikiwa za kutoridhisha kabisa.lakini sera mbaya ya nchi hiyo ikiwa ndio imechangia kwa kiasi kikubwa umasikini kwa wakazi wa Antananarivo.

4.BAMAKO, MALI.

Bamako ni mji mkuu wa Mali na makadirio ya watu milioni 1.4. Mji hutengeneza nguo, liyosindika nyama ,pamoja  na vyuma. Eneo la jiji hili limejaa mno uchafu, na inasadikika  kuishi katika jiji hili ni gharama kubwa sana, Bamako inakua wakati ukuaji wa idadi ya watu nayo inavyoongezeka. Sekta ya kilimo ya jiji hilo pia inafanya kazi vizuri zaidi. Katika miaka ya hivi karibuni, Saudi Arabia na China imewekeza Bamako kwa ajili ya maendeleo ya miundombinu na vituo vyao. Kadri mji unavyokua, uzalishaji wa umeme katika jiji hilo umeendelea  kuzalishwa kwa kutumia vyanzo vya maji. Bamako pia ina kituo cha  kkubwa cha kuzalisha maji katika nchi hiyo lakini pia imebidi wafunge mabomba kwa ajili ya kuvuta maji kutoka Mto Niger. Hata hivyo, upungufu wa maji bado huathiri zaidi kipindi cha kiangazi au majira ya joto. Vita kubwa nchini humo ni kuwaacha watu waishi bila chakula.

5.NIAMEY, NIGER.

Huu ni mji mkuu wa nchi ya Niger, Niamey ndi kituo cha utawala, kitamaduni na kiuchumi katika taifa la Niger. Wakati jiji lilijaribu kupiga hatua katika maendeleo, lilikumbana na changamoto ya mgawanyiko yenye utajiri miongoni mwa maeneo ya mijini na vijijini. Kutokana na mgogoro huu, Niamey inaendelea kudhoofika na kuifanya kuwa moja ya miji maskini zaidi duniani. Kwa kuwa idadi ya watu inaongezeka, viwango vya uhalifu kama uhamiaji haramu na matumizi ya madawa ya kulevya ukiendelea kushika kasi, utekaji nyara, ugaidi na ukiukwaji wa haki za wanawake ndio yamekuwa matukio yanayotikisa katika jiji hilo. Pia inasemekana kundi la kigaidi la Al Qaeda tayari limeanza kutngeneza himaya katika eneo hilo. Huku Ubaguzi, dini, na unyanyaswaji wa kimila ni vitu ambavyo viko kwa wingi jijini humo. Na kwa Sasa, changamoto kubwa inayowasumbua katika jiji hilo ni ukosefu wa chakula.

Haya ndio Majiji matano yenye hali mbaya ya kimasikini Duniani na hii ni kutokana na mtandao wa “We are the top ten” lakini katika majiji 10 yenye umasikini zaidi jiji la Dar Es Salaam likishika nafasi ya 7.

By Ally Juma.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents