Michezo

Yafahamu makundi ya kufuzu kombe la dunia 2022 Qatar, Tanzania yapangiwa timu hizi

Yafahamu makundi ya kufuzu kombe la dunia 2022 Qatar, Tanzania yapangiwa timu hizi

Cameroon au Ivory Coast haitashiriki katika kombe la dunia 2022 nchini Qatar baada ya timu hizo kuwekwa katika kundi moja katika raundi ya pili ya michuano ya kufuzu kwa kombe la dunia.

The indomitable lions ya Cameroon imeiwakilisha Africa mara saba katika kombe la dunia, huku Ivory Coast ikishiriki katika kombe hilo mara tatu.

Makundi mengine mawili yanashirikisha timu mbili ambazo zimeiwakilisha Afrika katika kombe la dunia.

Ghana na Afrika Kusini zitakutana katika kundi G pamoja na Zimbabwe na Ethiopia huku Misri na Angola pia zikikutana katika kundi F pamoja na Gabon na Libya.

Misri ilikuwa miongoni mwa wawakilishi watano wa Afrika katika kombe la dunia pamoja na Morocco, Nigeria, Senegal na Tunisia – na zote zinaamini kwamba zina fursa nzuri ya kufika katika raundi ya tatu na ya mwisho mnamo mwezi Novemba 2021.

Katika kundi B, Tunisia itakutana na Zambia, Mauritania na Equitorial Guinea huku Nigeria ikikutana na Cape Verde, Jamhuri ya Afrika ya kati na Liberia katika kundi C.

Kundi H Senegal itakabiliana na Congo, Namibia na Togo huku Morocco ikichuana na Sudan, na Guinea pamoja na Guinea Bissau katika kundi I.

Raundi ya kwanza ya mechi hizo za kimakundi itaanza Oktoba 2020 na kukamilika Oktoba 2021 kabla ya kufanyika kwa michuano ya muondoano Novemba 2021.

Ni washindi wa makundi hayo 10 pekee watakaosonga mbele katika mechi za muoandoano ambapo awamu mbili zitaamua wawakilishi watano wa kombe la dunia kutoka Afrika.

Mechi za kufuzu zilitarajiwa kuanza mwezi Machi lakini shirikisho la CAF likaahirisha michuano ya Afcon kutoka mwezi Juni hadi Januari.

Raundi ya kwanza ya mechi za kufuzu kwa kombe la dunia za Afrika ziliyafanya mataifa yanayoorodheshwa chini kushindana katika awamu mbili huku mshindi akisonga mbele na kujiunga na mataifa mengine 26 ambayo yataendelea katika raundi ya pili.

  • Kundi A: Algeria, Burkina Faso, Niger, Djibouti
  • Kundi B: Tunisia, Zambia, Mauritania, Equatorial Guinea
  • Kundi C: Nigeria, Cape Verde, Central African Republic, Liberia
  • Kundi D: Cameroon, Ivory Coast, Mozambique, Malawi
  • Kundi E: Mali, Uganda, Kenya, Rwanda
  • Kundi F: Egypt, Gabon, Libya, Angola
  • Kundi G: Ghana, South Africa, Zimbabwe, Ethiopia
  • Kundi H: Senegal, Congo, Namibia, Togo
  • Kundi I: Morocco, Guinea, Guinea-Bissau, Sudan
  • Kundi J: DR Congo, Benin, Madagascar, Tanzania

 

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents