Fahamu

Yafahamu mambo 10 muhimu usiyoyajua kuhusu michuano ya Afcon 2019, itakayofanyika Misri

Yafahamu mambo 10 muhimu usiyoyajua kuhusu michuano ya Afcon 2019, itakayofanyika Misri

Waandalizi wa michuano ya kombe la mataifa ya Akrika Misri waliorodheshwa katika kundi zuri ambalo huenda likawapendelea lakini mabingwa wengine kama vile Morroco , Ivory Coast na Afrika kusini waliwekwa pamoja katika kundi gumu. Hatahahivyo kuna mambo kumi usioyafahamu kuhusu kombe la Afcon 2019.

Kwa mujibu wa BBC. Haya ndio mambo 10.

1 – Misri itaandaa kwa mara ya tano kombe la Afcon. Walikuwa wenyeji wa kombe hilo 1959, 1974, 1986 na 2006, wakiibuka washindi katika michuano minne na kumaliza katika nafasi ya tatu katika mchuano wa mwisho.

2 – Ni mataifa matatu pekee, wenyeji Misri , Sudan na Ethiopia walioshiriki katika mchuano wa kwanza mnamo mwezi Februari 1957 na kulikuwa hakuna michunao ya kufuzu.

3 – 2019 Utakuwa mchuano wa kwanaza utakaoshirikisha mechi 24 , baada ya Caf kuamua kupanua mchuano huo ili kuimarisha ushindani.

4 – Taifa lililofanikiwa zaidi katika mashindano hayo ni Misri ikiwa na mataji saba ,ikifuatiwa na Cameroon {5} Ghana {4} Nigeria {3} , DR Congo na Ivory Coast {2 kila mmoja wao}

5 – Madagascar, Burundi na Mauritania zitakuwa zikishiriki kwa mara ya kwanza katika dimba hilo la 2019. Timu 12 hazajiwahi kufuzu katika kinyang’anyiro hicho , ikiwemo Jamhuri ya Afrika ya kati CAR, Chad Comoros, Djibouti, Eritrea, Eswatini, Gambia, Lesotho, São Tomé and Príncipe, Seychelles, Somalia na Sudan Kusini.

6 – Mshambuliaji wa Cameroon Samuel Eto’o anaongoza kwa wingi wa magoli, baada ya kufunga magoli 18 katika michuano 18 kati ya 2000 na 2010.

7 – Kipa wa Misri Essam el Hadary ndiye mchezaji mwenye umri mkubwa akiwa na miaka 44 na siku 21 kushiriki katika mchunao huo wakati alipocheza dhidi ya Cameroon 2017 mjini Libreville.

8 – Shiva N’zigou wa Gabon ndio mchezaji wa umri mdogo zaidi kushiriki na kufunga katika michuano hiyo. Alikuwa na umri wa miaka 16 na siku 93 wakati aliposhiriki katika michuano ya Afcon ya 2000 akifunga katika kichapo cha 1-3 dhidi ya Afrika Kusini

9 – Mchuano huo umebadilishwa siku zake za kufanyika ili kuzuia kugongana na kombe la dunia. Afcon kwa mara ya kwanza mwaka huu itafanyika katikati ya mwaka kinyume na ilivyokuwa awali ambapo ilikuwa ikifanyika mwezi Januari ili kuzuia mgongano wa mataifa na klabu za Yuropa.

10 – Mataji matatu tofauti yamekabidhiwa washindi katika historia ya mchunao huo. Kombe la sasa lilikabidhiwa 2002 na Misri iliibuka mshindi wakati huo baada ya kukamilisha ushindi wao wa mataji matatu 2010.

 

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents