Fahamu

Yafahamu mambo 10 ya kuzingatia, kabla ya kupanda Mlima Kilimanjaro – Video

Yafahamu mambo 10 ya kuzingatia, kabla ya kupanda Mlima Kilimanjaro - Video

Kinyume na fikra za watu wengi, kupanda mlima Kilimanjaro haihitaji mazoezi mengi sana. Waongozaji katika mlima Kilimanjaro ambao wanajulikana kama Guide wanaeleza sababu kwanini  wanawake na wanaume wenye kati ya umri wa mika 40 na 60 wanafanikiwa kupanda mlima Kilimanjaro kwa urahisi  zaidi kuliko vijana wenye umri kati ya 20 na 30.  Wanaeleza kwamba vijana wanaopanda mlima wanaanza na kasi sana na wanaishia kuchoka mapema, badala ya kwenda kidogo kidogo ili waweze kupanda hali ya kuwa wakiwa na pumzi ya kutosha.

Kwa maelezo hayo ili uweze kupanda mlima Kilimanjaro bila matatizo yoyote na ufanikiwe kufika kileleni na kuweze kushuka huku ukiwa na nguvu ya kutosha unashauriwa kufuata maelezo yafuatayo:-

1. Tembea, tembea na tembea zaidi

Hii ni muhimu sana kama unataka kufika juu kabisa. Utatembea sana kliko vitu vyote ukipanda mlima huu kwa hiyo, anza kutembea sana katika mazoezi yako ya kupanda Kilimanjaro.

Watu wengi wakiwa wanajiandaa kupanda Kilimanjaro wanasahau kwamba unafika kila kituo kwa kutembea masaa 5 au 8 kwa siku. Kawaida inachukua siku 6 au 8 kufika kileleni na kwa hiyo, utakuwa unatembea kwa masaa 5 au 7 kwa siku. Hakikisha unajiandaa kwa hii.

2. Chagua njia ya kupanda kabla

Ni kawaida kuwa na hamu kufika kwenye kilele ya Afrika, ila, inabidi ujihami na ukumbuke kwamba hakuna faida kuharakisha.

Kuharakisha inaweza ikakuletea madhara zaidi. Watu wanaotaka kupanda mlima ndani ya siku 4 au 5 wanaweza wakaamua kutumia njia ya kasi zaidi.Ila, wanasahau kukumbuka kwa mwili inahitaji muda wa kujizoesha kwa viwango vya chini vya oksijeni, kadri unavyopanda. Hii ndio maana watu wengi wanaishia kuugua kadri wanavyopanda mlima na hivyo, kushindwa kuupanda. Badala yake, pitia njia zote na pia soma maoni ya watu juu ya njia hizi.

Utapata mtazamo wa njia itakayokufaa ili upande mlima kwa furaha na mafanikio. Kulazimishwa kurudi inasikitisha, hasa ikiwa kwamba afya yako ni nzuri ila hukuwa na subira na hivyo ukakosea kwa kutumia njia ya kasi na ukaishia kuumwa. Kumbuka, haraka haraka haina Baraka.

3. Maji ni rafiki yako wa karibu!

Hupendi kunywa maji? Anza kujizoesha kunywa! Kuwa na hidarati ni lazi kama una matumaini ya kufika mbali. Mwili wako unakosa hidarati kwa kasi zaidi kwa sababu ya mwinuko na hii inaweza ikasababisha usikia kizunguzungu au upate maumivu makali ya kichwa.

Watu waliofanikiwa kufika kileleni na kushuka kwa usalama wanapendekeza unywe lita 5 za maji kwa siku. Hii inaweza ikaonekana kuwa ngumu kufanya, ila ni lazima kama unatarajia kufika kileleni.

4. Fanya mazoezi kwenye sehemu zenye milima na uongeze uzito

Ukiwa unapanda mlima Kilimanjaro, utakuwa umebebabegi nzito na utabidi upande milima mikali pamoja na begi hiyo.

Njia moja ya kujiandaa kwa hii nikutembea kwenye sehemu yenye milima mikali karibu na nyumbani, ukiwa umevaa begi hiyo. Kumbuka kuanza na mlima isiyokali sana ila ukali uongezeka kadri unavyo fanya mazoezi. Pia, ongeza uzito kwenye begi kadri unavyofanya mazoezi.

5. Kumbuka lengo lako

Unajua kwamba mwanamke mwenye umri zaidi aliyewahikupanda Kilimanjaro alikuwa na miaka 86? Angela Vorobeva alithibitisha kwa watu wengi waliokuwa na wasiwasi wa kupanda mlima huu kwamba mtu yoyote anaweza kuupanda. Kuwa na afya bora sio kila kitu.

Unavyopanda Kili – jina la kifupi la Kilimanjaro ilyopewa na wakazi wa hapo – ni lazima ukumbuke sababu yako ya kuupanda na utakavyojisikia ukikamilisha lengo lako.

Hii itakusaidia sana ukijisikia kukata tamaa. Tunatumaini kwamba sababu yako ya kupanda Kili ni zaidi ya kuweza kujisifia kwamba umepanda mlima Kilimanjaro.

6. Vaa kwakuzingatia mazingira

Ni lazima uwe na mavazi sahihi kama hutaki kuganda au kupata ugonjwa wa mwinuko. Utafiti mkubwa wa glovu bora, begi bora, viatu vizuri na hata chupi zinasaidia kuhakikisha kwamba unajisikia vizuri kiasi ukipanda na ukishuka.

Hutaki kuwa na wasiwasi juu ya miguu baridi, mdomo uliokatika au kutokuwa na betri kwa ajili ya tochi, ukiwa umeshachoka sana. Rahisisha maisha yako kwa kuwa na mavazi sahihi.

7. Jiandae na maisha ya kawaida sana

Isikushangaze kwamba kati ya hizo siku 6 au 8 utakazo kuwa unapanda mlima, hutaweza kuoga. Wanawake, naomba msahau swala la vipodozi kabisa! Kwa hiyo, zoea kuisha kwa kawaida na usihofie chochote. Wote mtakumbwa na tatizo hii.

Watu wengine wanapata wakati mgumu kwenye maisha ya kambi. Kabla ya kwenda kupanda mlima, jaribu kupanga safari ndogo ya kambi ili upate mazoefu zaidi ya kambi.

8. Ugonjwa wa Mwinuko ni adui wako

Ni ngumu sana kuepukana na ugonjwa wa mwinuko.Pia, wachukuzi wanaamini kwamba watu wanaofanya mazoezisana wana nafasi kubwa ya kuumwa sana kwa kuwa wanataka kuharakisha ili waongeze kundi wanalopanda nalo.

Kuharakisha sio njia ya kufanikiwa kufika kileleni na kushuka bila kuumwa. Mwili inahitaji muda wakujizoesha na viwango vya chini vya oksijeni na kutembea polepole inakupa muda kuzoea kupumua kwa uzito zaidi ili kujizoesha na viwango hivi.

Jiandae kupata maumivu ya kichwa, ukosefu wa hidrati na kutapika. Tegemea vyote vitokee kwa sababu ya mabadiliko ya mwingo na unachoweza kufanya ili kupunguza ukali yao ni kupanda pole pole na kunywa maji mengi.

9. Jiepushe na Jua

Kadri unavyopanda, mionzi ya jua yanakuwa makali zaidi zenye madhara zaidi. Kwa hiyo ukitembea, tembea kwenye sehemu za kivuli. Pia, kuunguzwa kwa jua haiathiri muonekano wako tu lakini pia, huathiri nafasai yako ya kufika kileleni. Mwili wako unakosa hidrati zaidi ikiwa imeunguzwa na jua, kwa hiyo beba mafuta ya kuzuia makali ya mionzi ya jua.

10. Furahi

Kupanda Kilimanjaro ni kitu cha kukumbuka maisha yako yote. Kwa wengi waliofanikiwa kuupanda, ile safari ya kufika kileleni ndio kinachowafurahisha sana, zaidi ya kufika kileleni kwenyewe. Utapata hisia mbalimbali ukiwa unaupanda ila utaona mandhari ya kuvutia kwa kiwango isiyo kawaida. Kwa hiyo, kumbuka kufurahia safari yote ya kufika kwenye kilele cha Afrika. Ni kitu cha ajabu.

NB: Mwongozaji wako (Guider) wa kupanda mlima atachangia kwa nafasi kubwa sana katika safari yako kwa hiyo, pata mwongozi bora kabla ya kupanda.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents