Michezo

Yafahamu mambo 8 yaliyojitokeza katika mchezo wa PSG dhidi ya Manchester United ambayo ni nadra kutokea katika michuano ya UEFA

Katika michuano mikubwa kabisa barani Ulaya ya UEFA imeendelea kuweka historia kwani tangu ianzishwe mnamo mwaka 1955 na kufanyiwa marekebisho mwaka 1992 takribani miaka 64 sasa ambayo huwaga ianshirikisha timu 32 kutoka katika mataifa wanachama barani Ulaya huku klabu ya real Madrid wakiwa ndio vinara wa kutwaa taji hili wakitwaa kwa nyakati 13 na mara ya mwisho kutwaa ni 2018/19 ambapo wmefanikiwa kuchukua kwa mara tatu mfululizo.

PARIS, FRANCE – MARCH 06: Angel Di Maria of PSG crosses the ball during the UEFA Champions League Round of 16 Second Leg match between Paris Saint-Germain and Manchester United at Parc des Princes on March 06, 2019 in Paris, . (Photo by Julian Finney/Getty Images)

Usiku wa kuamkia leo imefanyika tena michuano hiyo ambapo ilifanyika michezo miwili mmo0ja ukichezwa nchini Ufaransa kati ya wenyeji PSG na wageni kutoka England Manchester United, lakini pia mchezo mwingine ulikuwa ni kati ya Porto kutoka nchini Ureno na AS Roma kutoka nchini Italia na katika michezo hiyo timu mbili zimefanikiwa kusonga mbele katika michuano hiyo ambapo Manchester United wamefanikiwa kuibwaga PSG katika michuano hiyo kwa ushindi wa goli 3-1 na katika mchezo wa kwanza United walifungwa goli 2-0 nyumbani kwao hivyo United wamefanikiwa kusonga mbele kwa tofauti ya magoli huku katika mchezo wa Porto na AS Roma, Porto wamefanikiwa kuibwaga Roma kwa kuifunga pia goli 3-1 na katika mchezo wa kwanza Roma walishinda goli 2-1 hivyo Porto wamepita kwa tofauti ya magoli pia.

Katika mchezo ambao ulivuta hisia za wapenda soka wengi zaidi duniani ni ule ambao ulifanyika nchini Ufaransa ambapo United walikuwa wageni wa PSG na PSG kutolewa kwenye michuano hiyo kwa kufungwa goli 3-1, yafuatayo ni mambo 8 yaliyojitokeza katika mchezo huo ambayo ni nadra sana kutokea katika michuano mikubwa ya UEFA lakini pia havikuwahi kutokea katika historia ya timu hizo mbili:-

  1. Manchester United imekuwa ndio timu ya kwanza katika historia ya Ligi ya Mabingwa kufuzu kwa mechi ya pili baada ya kupoteza mechi ya kwanza nyumbani kwa magoli mawili au zaidi.
  2. PSG ilikubaliana kufungwa goli tatu kati ya mashuti manne ya kushambulia ambayo yalitokea katika mchezo ya hatua hii ambazo zimepelekea timu hiyo kuondolewa katika hatua ya mwisho ya 16 bora ikiwa ni msimu wa tatu wa Ligi ya Mabingwa.
  3. Goli la kwanza la mshambuliaji wa Manchester United Romelu Lukaku baada ya sekunde 111 limekuwa goli la Man Utd la haraka zaidi katika mechi ya klabu katika michuano ya Ligi ya Mabingwa tangu Wayne Rooney alifunga baada ya sekunde 63 dhidi ya Bayern Munich Machi 2010.
  4. Goli la ushinda la Marcus Rashford ambaye alifunga mkwaju wa penati ndiyo limekuwa goli la kwanza kwake aliyefanikiwa kufunga katika mechi ya ushindani akiwa Manchester United.
  5. PSG imepoteza mechi saba kati ya 12 ya mwisho katika Ligi ya Mabingwa barani Ulaya (W4 D1), ikiwemo michezo yao miwili ya mwisho waliyocheza katika uwanja wao wa Parc des Princes.
  6. Tangu mchezo wa kwanza wa kocha mpya Ole Gunnar Solskjaer mnamo Desemba 22, ni Manchester City tu waliofanikiwa kushinda michezo (15) wakiwa ndio wameshinda mechi nyingi zaidi katika mashindano yote ikifuatiwa na Man Utd waliofanikiwa kushinda michezo (14) katika timu zilizopo katika ligi za juu za 5 barani Ulaya.
  7. Manchester United sasa imefanikiwa kufunga magoli 21 katika michezo mfululizo wakiwa ugenini katika mashindano yote, sawa na rekodi ya klabu iliyowekwa kati ya Novemba 1956 na Septemba 1957 chini ya Sir Matt Busby.
  8. Mason Greenwood ndio amekuwa mchezaji mdogo zaidi kuonekana na kuichezea Manchester United katika Ligi ya Mabingwa, akiwa na umri wa miaka 17 na siku 156, amefanikiwa kuvunja rekodi ya Gerard Pique aliyekuwa na miaka 17 na siku 310.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents