Michezo

Yafahamu mataifa 12 kutoka barani Afrika yaliyosimamisha masuala ya michezo katika nchini zao kisa Corona

Yafahamu mataifa 12 kutoka barani Afrika yaliyosimamisha masuala ya michezo katika nchini zao kisa Corona

Kutokana na maambukizi ya virusi vya Corona vinavyoendelea kusambaa kote duniani ambapo yalianzia katika taifa la China na sasa virusi hivi vimetapakaa karibia dunia nzima kwani katika kila bara kwa sasa kuna maambukizi ya corona.

Ikiwa China ndio nchi ya kwanza kuvivumbua virusi hivyo na kwa sasa ikiwa na kesi za Corona takribani 80881 huku wanaokadiriwa kupona wakiwa ni 61644 na walipoteza maisha wakiwa ni 3226 huku wakifuatiwa na taifa la Italia lenye kesi 27980 waliopona wakiwa 1045 na walipoteza maisha wakiwa ni 2158 na taifa la 3 kwa kuwa na kesi nyingi za Corona likiwa ni Irani lenye kesi 14 991 walipona wakiwa ni 2959 na walipoteza maisha wakiwa ni 853.

Kwa upande wa bara la Afrika taifa linaloongoza kwa kuwa na kesi nyingi za Corona likiwa ni Misri lenye kesi166 huku waliopoteza maisha wakiwa ni 4 na walipona wakiwa 27, Misri inafuatiwa na taifa la Afrika Kusini lenye kesi 64 huku mpaka hivi sasa hakuna aliyepona wala aliyepoteza maisha taifa la 3 ni Algeria lenye kesi 60 na walipoteza maisha wakiwa 4 na mpaka hivi sasa kukiwa hakuna aliyepona hata mmoja.

Kutoka na maambukizi haya mataifa mengi sana duniani yamesimamisha baadhi ya shughuli zao huku mengi yakisimamisha kila kitu na kukataza watu kutoka nje ya nyumba zao na wengine wakifanyia kazi wakiwa majumbani kwao.

Katika bara la Afrika licha ya kuwa bado hakuna kesi nyingi za wagonjwa wa Corona tofauti na mabara mengi kuna mataifa ambayo yamesimisha shughuli zote za michezo.

Mpaka hivi sasa yamefikia mataifa 12 yaliyosimisha shughuli zote za kimichezo na mataifa hayo ni.

 

Egypt

DR Congo

Morocco

Kenya

Gabon

Sudan

Botswana

Ghana

Algeria

South Africa

Ethiopia

Sudan

Mbali na mataifa hayo pia shirikisho la michezo barani Afrika limesimisha baadhi ya amshindano yanayoendeshwa chini ya shirikisho hilo.
By Ally Juma.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents