Bongo5 Exclusives

Yahoo yanunua application iliyotengenezwa na mtoto wa miaka 17 kwa mamilioni ya dola

Mbunifu wa app ya habari iitwayo ‘Summly’, Nick D’Aloisio, 17 amekuwa milionea baada ya Yahoo kuinunua application yake.

Nick_D_Aloisio_1698346a

Japo haijulikani ni kiasi gani hasa alicholipwa lakini ni mamalioni ya dola.App hiyo itaanza kutumika kwenye products za Yahoo. Summly huchukua habari za mtandaoni na kuzifupisa kuwa na maneno 400 ambazo ni rahisi kusomwa kwenye simu za mkononi.

Pia, mtoto huyo atakuwa mwajiriwa wa Yahoo mwenye umri mdogo zaidi.Nick aliitengeneza app hiyo akiwa na umri wa miaka 25 na kupata uwekezaji kutoka kwa kampuni ya bilionea wa Hong Kong, Li Ka Shing iitwayo Horizons Ventures na kupata shavu kutoka kwa mastaa kama Stephen Fry, Yoko Ono na Ashton Kutcher waliowekeza kwa zaidi ya paundi milioni moja.

App hiyo kwaajili ya simu za iPhone ilianzishwa December 2012 na Summly ilifanya kazi na mitandao zaidi ya 250 duniani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents