Technology

Yahoo yanunuliwa na kampuni ya Verizon kwa dola bilioni 5

Kampuni ya internet ya Marekani, Yahoo imenunuliwa na kampuni ya mawasiliano ya Verizon Communications kwa dola bilioni 5, fedha taslimu.

Yahoo

Yahoo itaunganishwa na AOL, kampuni nyingine ya internet iliyopoteza umaarufu ambayo nayo ilinunuliwa mwaka jana na kampuni hiyo. Hata hivyo dili hilo halijumuishi hisa za thamani ilizonazo kwenye kampuni ya China, Alibaba.

121128_marissa_mayer

CEO wa Yahoo, Marissa Mayer

Fedha hizo ni ndogo zaidi kuliko dola bilioni 44 ambazo kampuni ya Microsoft ilitaka kuinunua Yahoo mwaka 2008. Yahoo iligoma kununuliwa kwa kiasi hicho cha fedha. Enzi za umaarufu wake, Yahoo ilikuwa na thamani ya dola bilioni 125.

CEO wa saba na wa mwisho wa Yahoo, Marissa Mayer, anadaiwa kuwa ataondoka baada ya dili hilo huku akilipwa kiinua mgongo cha dola milioni 50.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents