Michezo

Yaliyojiri baada ya PSG kutupia mabao 5 Uefa, Mbappe ashambuliwa

By  | 

Mchezaji wa matajiri wa Ufaransa klabu ya Paris St-Germain na timu ya taifa ya Ufaransa, Kylian Mbappe ameshambuliwa na shabiki wa timu ya Celtic wakati wa mchezo wao wa kwanza wa klabu bingwa barani Ulaya uliyochezwa hapo jana siku ya Jumanne.

Tukio hilo limetokea katika dakika 45 za kipindi cha kwanza cha mchezo huo wakati PSG ikiwa inaongoza kwa mabao 5 katika dimba hilo la Celtic Park ndipo shabiki wa Celtic akaingia uwanjani na kumshambulia kwa teke Mbappe.

Kwa tukio hilo Celtic imeshtakiwa na FIFA kwa shabiki wake kujaribu kumpiga mchezaji huyo.

Wakati hayo yakijiri matajiri wa Ufaransa timu ya PSG inakabiliwa na shtaka la mashabiki wake kuvunja viti vya uwanajani kesi ambayo inatarajiwa kutangazwa na  kitengo cha maadili na nidhamu katika Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Ulaya ‘UEFA’ Octoba 19 mwaka huu.

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments