Burudani

Yamoto Band kufunga mwaka na wimbo mpya ‘Mama’

Kundi la muziki linalofanya vizuri na wimbo wake Cheza Kimadoido, Yamoto Band wanajipanga kufunga mwaka na wimbo wao mpya uitwao Mama.

Yamoto band

Akizungumza na Bongo5 hivi karibuni meneja wa Yamoto Band, Said Fella alisema kabla wasanii hao hawajasafiri kuelekea nchini Marekani kwaajili ya show tatu, wataachia wimbo mpya utakaofunga mwaka.

“Tarehe 25 mwezi huu watasafiri kuelekea Marekani kwaajili show. Tarehe 27 watafanya show ya kwanza, watafanya tena Houston halafu watamalizia Washington DC,” amesema. “Lakini kabla ya kusafiri nimeona waachie kazi mpya kabla ya kuondoka. Ngoma inaitwa Mama na tumemshirikisha dada mmoja alikuwa 5 Stars. Wakati ule akina marehemu Kijoti walivyopata ajali na huyu dada alikuwepo alikuwa anaitwa Rena Mohamed yeye ndio kasimama kwenye chorus na tumemshirikisha huyo ili tuwakumbushe watu kwamba kuna watu wameshafanya kazi nzuri kwenye muziki.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents