Burudani

Yamoto Band kuvunja ukimya

Jumamosi hii katika Tamasha la Fiesta 2017 lililofanyia Leaders Club tulishuhudia wasanii wa Kundi la Yamoto Band wakiungana pamoja kama zamani na kufanya show ya pamoja na kuleta msisimko mkubwa kwa mashabiki waliojitokeza ukumbini hapo.

Wasanii wa kundi hilo kwa sasa kila mmoja anafanya kazi kivyake huku Aslay pamoja na Beka Flavour wakionekana kufanya vizuri kutokana na vibao vyao walivyovitoa hivi karibuni kupendwa zaidi na mashabiki.

Akiongea na mashabiki waliojitokeza kwenye tamasha hilo, Aslay amewataka mashabiki kujipanga kwaajili ya kibao kipya cha kundi hilo.

“Asanteni sana mashabiki kwa upendo wetu kuna kitu kipya tunawaandalia,” alisema Aslay baada ya kumaliza show yao hiyo.

Katika show hiyo Maromboso ndiye msanii pekee wa kundi hilo aliyekosekana huku baadhi ya wadau wakidai muimbaji huyo anajiunga na WCB ndio maana ameshindwa kuonekana tena akiwa pamoja na kundi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents