Burudani

Yamoyoni ya Amini yachanja mbuga

Msanii wa muziki, Amini amefunguka kuzungumzia mafanikio ya wimbo wake mpya Yamoyoni aliouachia wiki chache zilizopita.

Akiongea Bongo5 wiki hii, Amini amedai wimbo wake huo umeweza kufanya vizuri zaidi kwa muda mfupi kuliko nyimbo zake nyingine.

“Kusema kweli Yamoyoni umekuwa wimbo mkubwa sana, umeingia kwenye chart mbalimbali za radio kwa sababu kazi ni nzuri. Pia naweza kusema katika nyimbo zangu ambazo nimetoa hivi karibuni Yamoyoni ni wimbo ambao umesambaa kuliko nyimbo zangu zilizopita kwa muda mfupi,”

Muimbaji huyo amedai ukiachana na Yamoyoni ambayo inafanya vizuri, anajipanga kuachia kazi mpya.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents