Michezo

Yanga ifanye kazi ya ziada Kombe la Shirikisho Afrika.

Yanga ifanye kazi ya ziada Kombe la Shirikisho Afrika.

Klabu ya Dar Es Salaam Young Africa (Yanga) kutoka nchini Tanzania tayari imewasili nchini Kenya kwa ajili ya mchezo wa duru ya kwanza katika michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Gor Mahia.

Mchezo huo wa Ufunguzi unaotarajiwa kupigwa kesho Julai 18, 2018 Yanga watakuwa na kibarua kigumu dhidi ya mabigwa hao wapya wa SportPesa Super Cup, hii ni kutokana na kuwa na maandalizi hafifu na baadhi ya wachezaji wake kuihama klabu hiyo kama Donald Ngoma aliyejiunga na Azam FC vile vile mfungaji wao tegemezi Obrey Chirwa aliyetimkia nchini Misri.

Lakini kwa upande wa Gor Mahia wao wameweza kujiandaa katika mashindano mbalimbali baada ya kumalizika kwa Ligi Kuu nchini Kenya kwa kushiriki katika michuano kadhaa ikiwemo ya SportPesa Super Cup na CECAFA Kagame Cup.

Baadhi ya wadau waliozungumzia mchezo huo ni mchezaji wa zamani wa Yanga, Ally Mayay ambaye kwa sasa ni mchambuzi wa masuala ya soka katika vituo mbalimbali vya utoaji habari. aliongea hayo wakati wa Uchambuzi katka moja ya mchezo ambao Gor Mahia walikuwa wakicheza  michuano ya Cecafa Kagame Cup kupitia kituo cha Azam Tv wakati akiisifia timu ya Gor Mahia kuwa ni  timu yenye maandalizi mazuri na pia ni klabu iliyojiimarisha vya kutosha.kwani mpaka siku ya mchezo Gor Mahia watakuwa na nguvu zaidi waliyotoka nayo katika hii Michuano.

Hata hivyo, licha ya klabu hiyo kutokufanya maandalizi ya kutosha lakini pia wamekuwa katika wakati mgumu kiuchumi.

Klabu ya Yanga inashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya kutolewa katika kome la Klabu Bingwa barani Afrika na klabu ya Township Rollers kutoka nchini Botswana mapema mwezi machi mwaka huu.

By Ally Jei.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents