Michezo

Yanga imetwaa ubingwa wa kombe shirikisho

Klabu ya soka ya Yanga, imetwaa ubingwa wa kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Kombe la Azam Sports Federation Cup (ASFC) kwa kuichapa Azam, kwa mabao 3-1.

2X6A9536-1

Mchezo huu uliopigwa kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam, ulishudia kikosi cha Yanga, ilipata ushindi wake kupitia kwa magoli ya mshambuliaji Amisi Tambwe aliyefunga bao la kwanza katika dakika ya tisa ya kipindi cha kwanza kisha akaongeza bao la pili katika dakika ya 47 ya kipindi cha pili.

Katika dakika ya 81 winga Deus Kaseke, alihitimisha kazi kwa kufunga bao la tatu baada ya kuunganisha krosi ya Simon Msuva.Bao la kufutia machozi la Azam,liliwekwa kambani na mshambuliaji Didier Kavumbagu.

Licha ya Yanga kushinda mchezo huu wa fainali Azam ndio wataiwakilisha Tanzania katika michuano ijayo ya kombe la shirikisho huku Yanga wakiwakilisha katika michuano ya klabu bingwa Africa.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents