Burudani ya Michezo Live

Yanga kuchele, kamati zakutana kujadili ujenzi wa uwanja mpya, ramani hii hapa (+Picha)

Wajumbe wa kamati ya Ujenzi na Miundombinu na baadhi ya wajumbe wa kamati ya Utendaji wa Mabingwa wa kihistoria wa ligi kuu soka Tanzania Bara Young Africans wamekutana hapo jana kujadili masuala mbalimbali ikiwemo ujenzi wa Uwanja wao uliyopo Kigamboni.

Kamati hizo za Yanga zilikutana hapo jana ambapo Wanajangwani hao walitoa taarifa kuhiyo kupitia akaunti yao ya kijamii ya Instagrama huku wakionyesha baadhi ya picha za uwanja huo na baadhi ya walioshiriki kikao hicho.

”Mambo yanakwenda. Wajumbe wa Kamati ya Ujenzi na Miundombinu ya Yanga, na baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Utendaji wamekutana leo kujadili masuala mbalimbali ikiwamo hatua za awali za ujenzi wa Uwanja na Academy ya Yanga huko Kigamboni.”- Imeandika Yanga

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda aliwapatia Yanga SC eneo lenye ukubwa wa hekari saba pamoja na hati ya umiliki kwa klabu hiyo kwa ajili ya ujenzi wa uwanja na matumizi mengine, ikiwa ni ahadi aliyoitoa wakati wa hafla ya harambee ‘Kubwa Kuliko’ ya uchangiaji wa timu hiyo Juni 5.

Eneo hilo lipo umbali wa Kilomita 14 kutoka Daraja la Mwalimu Nyerere na umbali wa Mita 200 kutoka Barabara kubwa.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW