Michezo

Yanga Kuchuana Afrika Magharibi

 

Uongozi wa klabu ya Yanga umesema kuwa utatafuta mechi kadhaa za kimataifa za kirafiki kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya kombe la shirikisho (CAF) kwa ajili ya kujiweka sawa ambapo timu za Afrika Magharibi ndizo walizolenga kukabiliana nazo katika kujipima uwezo wao.

kwa mujibu wa msemaji wa klabu hiyo, Louis Sendeu, kocha mkuu Kosta Papic ndiye anayengojewa kutoka Serbia alipoenda kwa ajili ya mapumziko baada ya mzunguko wa kwanza wa ligi kuu ya Vodacom kisha watajadiliana juu ya timu za kukabiliana nazo.

‘Tutakuwa na mechi kadhaa za kimataifa ambapo tumepanga kutafuta timu kutoka nchi za Afrika ya Magharibi ambazo ni pamoja na Ivory Coast,Ghana,na nyinginezo hivyo tutaangalia ni timu gani itaweza kuja kucheza na timu yetu.’

‘Kikosi kinatarajiwa kurudi kambini Novemba 26 kwa ajili ya kujiandaa na mzunguko wa pili pamoja na michuano ya CAF ambapo lengo kubwa ni kufanya vizuri katika michuano hiyo.”alisema Sendeu.

Watatumia usajili wa dirisha dogo kwa ajili ya kukiiimarisha kikosi kwa ajili ya michuano hiyo ili waweze kuwa na timu bora na imara zaidi itakayotoa ushindani wa aina ya juu zaidi katika michuano.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents