Michezo

Yanga kuiwekea kambi Simba visiwani Zanzibar

Mabingwa wa kihistoria wa Ligi Kuu Bara klabu ya Dar es salaam Young Afrika inatarajia kufunga safari na kwenda Kisiwani Pemba Zanzibar kuweka kambi ya wiki moja kwa ajili ya maandalizi  ya wiki moja kujipanga kumkabili Mnyama Simba katika mchezo wa Ngao ya jamii unaotarajiwa kuchezwa  Agosti 23 mwaka huu.

Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Charles Mkwasa amesema kuwa kikosi cha Yanga kinatarajia kuondoka Jijini Dar es Salaam  mara  baada ya mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Ruvu Shooting utakaochezwa Uwanja wa Taifa siku ya  Jumamosi na kisha kuweka kambi Zanzibar ambapo watapata fursa ya kucheza mchezo mmoja wa kirafiki wakiwa visiwani humo.

 

Wachezaji wa Kikosi cha Dar es salaam Young Africans

By Hamza Fumo

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents