Michezo

Yanga kukabidhiwa kombe la Vpl moja kwa moja ?

Ligi kuu soka Tanzania Bara imendelea siku ya leo, ambapo mashabiki na wadau wa mchezo wa mpira wa miguu nchini wameshuhudia viwanja kadhaa vikiwaka moto, lakini macho na masikio ya walio wengi hii leo yalikuwa yakielekezwa huko Jangwani kunako klabu ya Yanga.


Timu ya Yanga ikisherekea baada ya kukabidhiwa Ubingwa msimu wa 2014/15

Klabu ya soka ya Dar es salaam Young Afrika hii leo walitupa tena karata yao kuivaa timu ya Jiji, klabu ya Mbeya City ya mkoani Mbeya katika mchezo uliopigwa katika Dimba la Taifa jijini Dar es salaam, ikiwa ni mchezo ambao wenyeji, klabu ya Yanga iliweza kuchomoza na ushindi wa jumla ya magoli 2 kwa 1 , magoli yaliyowekwa kimyani na Simon Msuva pamoja na Haruna Nionzima kwa upande Yanga huku goli pekee la kufutia machozi kwa upande wa Mbeya City likifungwa na Chirwa .

Kama klabu ya Yanga itanyakuwa Ubingwa wa ligi kuu ya Vpl msimu huu, basi itakuwa imejiwekea historia ya kuchukua kombe hili mara tatu mfululizo.


Timu ya Yanga ikisherekea baada ya kukabidhiwa Ubingwa msimu wa 2015/16

Kwa ushindi huo, sasa klabu ya Yanga imerejea tena kileleni mwa ligi na hivyo kuongoza ligi kwa jumla ya alama 65 sawa na Mahasimu wao klabu ya Simba Sc, ambao wana alama sawa tofauti ya magoli ya kufungwa na kushinda.

Ligi kuu soka Tanzania bara msimu huu imekuwa na ushindani mkubwa hasa kwa vilabu hivi viwili vinavyowania ubingwa. Mpaka sasa, ni ngumu kubashiri Bingwa wa msimu huu atakuwa nani licha ya kusalia michezo michache kwa kila timu, wana jangwani Dar Young Afrika wana michezo miwili mkononi kabla ya ligi kumalizika huku kwa upande wapili wa klabu ya Simba Sc nao wakiwa wamesaliwa na mchezo mmoja pekee.

Yanga na Simba zinalingana alama, huku kila mmoja akiwa amejikusanyia jumla ya alama 65. Licha ya klabu ya Yanga kuwa na michezo miwili ni ngumu kubashiri Bingwa wa Msimu huu wa mwaka 2016/17 atakuwa nani. Je Ni Yanga Tena na kuondoka nalo moja kwa moja ?, ama Simba Sc baada ya kulikosa misimu mitano ?

Katika michezo mingine iliyopigwa hii leo, Matajiri wa Sukari, klabu ya Mtibwa Sugar imechomoza na ushindi mnono wa magoli 4 kwa 2 dhidi ya klabu ya Mwadui Fc,JKT Ruvu wakikubali kipigo cha goli 1 kwa 0 kutoka kwa klabu ya Majimaji, Prison ikiibuka na ushindi wa magoli 2 kwa 1 dhidi ya klabu ya Ndanda ya mtwara.

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents