Michezo

Yanga kuwakosa wachezaji muhimu V Simba SC Agosti 23

Mabingwa wa kihistoria wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara klabu ya Dar es salaam Young Africans inatarajia kuwasili Dar esa laam kesho ikitokea Visiwani Pemba ilipokuwa imeweka kambi yake ya wiki kadhaa.


Young Africans inatarajia kucheza mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya mahasimu wake Simba SC unaotarajiwa kupigwa katika dimba la Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam ikiwa unaashiria kuanza kwa ligi kuu ya Vodacom ambayo itaanza rasmi Agosti 26 siku tatu baada ya mchezo huo wa wawatani wa jadi.

Joto la Ilala ‘Derby’ Simba v Yanga lapanda
Katika kuelekea katika mchezo huo wa kihistoria Yanga imetoa taarifa ya kuwakosa wachezaji wake muhimu, mshambuliaji raia wa Zambia, Obrey Chirwa, Benno na Geofrey Mwashiuya ambao wanasumbuliwa na majeraha.

By Hamza Fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents