Uncategorized

Yanga na mpango wa kukusanya Bilioni 1.5, kikao kizito cha kamati na uhamasishaji chafanyika

Mabingwa wa kihistoria wa ligi kuu soka Tanzania Bara Yanga SC hii leo wameendelea na harakati zao za kuhakikisha wanatengeneza mikakati madhubuti ya ukusanyaji michango kutoka kwa wanachama wao, mara baada ya kufanya kikao cha uzinduzi wa kampeni hiyo.

Kupitia akaunti yao ya kijamii ya Instagram, Yanga imeeleza kwa uchache kikao chao ambapo ni pamoja na mikakati.

”Kikao cha kwanza cha kamati ya uzinduzi na uhamasishaji rasmi wa kampeni ya kuichangia timu awamu ya pili kimefanyika,” imesema Yanga SC kupitia akaunti yake ya Instagram.

Yanga ambao ndiyo klabu pekee iliyofanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu mara tatu mfululizo na maranyingi zaidi wameongeza ”Pamoja na mipango na mikakati mipya mizuri iliyowekwa, kwenye kikao hicho, Mwenyekiti wa kamati hiyo Mh. Antony Mavunde aliainisha mpango mpya wa kukusanya kiasi cha Tsh 1.5B kutoka kwa wanachama na mashabiki wa Yanga SC mikoa yote nchini.”

Wakati Yanga inapanga kuendelea kutembeza bakuli kama wanavyosema wenyewe upande wa pili wa shilingi kwa mahasimu wao Simba inazidi kung’ara kimataifa hii ni mara baada ya kufanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya klabu bingwa barani Afrika inayosimamiwa na Shirikisho la soka barani Afrika Caf.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents