DStv Inogilee!

Yanga na Simba zaingiza Mil. 342 mechi ya watani wa jadi, timu mwenyeji yapata kiasi hiki kwenye mgawanyo wa fedha

Mchezo namba 270 wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara uliozikutanisha Young Africans na Simba uliochezwa Jumamosi Februari 16,2019 kwenye Uwanja wa Taifa umeingiza jumla ya shilingi Milioni 342,825,000.

Mchezo huo uliingiza jumla ya watazamaji 41,266. VIP A waliingia Watazamaji 546 kwa kiingilio cha Shilingi 30,000 na kupatikana jumla ya shilingi 16,380,000,VIP B na C waliingia Watazamaji 3,185 kwa kiingilio cha shilingi 20,000 ikapatikana jumla ya shilingi 63,700,000,Majukwaa ya rangi ya Machungwa,Bluu na Kijani waliingia Watazamaji 37,535 kwa kiingilio cha shilingi 7,000 imepatikana jumla ya shilingi 262,745,000

Mgawanyo wa mapato

VAT 52,295,338.98

Selcom 15,170,006.25

TFF 13,767,982.74

Uwanja 41,303,948.22

Young Africans 165,215,792.86

Gharama za mchezo 19,275,175.83

TPLB 24,782,368.93

BMT 2,753,596.55

DRFA 8,260,789.64

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW