Makala

Yanga SC na Singida United kumuweka njiapanda Mwigulu Nchemba

Mwanachama na shabiki wa klabu ya Yanga na Singida United, Mwigulu Nchemba ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani Jumamosi hii atakuwa kwenye kipindi kigumu wakati timu hizo zitakapokutana katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Yanga SC itashuka dimbani katika Uwanja wa Namfua  kucheza na Singida United mchezo utakao kuwa wa kukata na shoka hali itakayomfanya Nchemba kuwa katika wakati mgumu kutokana na mahaba aliyokuwa nayo dhidi ya timu hizo mbili.

Wakati nyasi za Uwanja wa Namfua zikitarajiwa kuwaka moto dhidi ya mahasimu hao wawili walioonja ufundi wa kocha Hans Pluijm , ndivyo mapigo ya moyo ya mbunge huyo wa Iramba yatakavyokuwa  juu siku hiyo ya Jumamosi.

Marakadhaa Nchemba ameonekana katika mahaba mazito na timu ya Singida United hasa kujitolea michango yake kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri.

Mpaka sasa wapenzi wa soka hawanajibu kamili la upande gani mdau huyo wa michezo atashabikia siku hiyo baina ya Yanga SC au Singida United.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents