Michezo

Yanga SC ,Simba SC na Azam FC kutafuta point tatu muhimu wiki hii

By  | 

Duru la tatu la Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara linatarajiwa kuendelea tena hapo kesho tarehe 15 kwa wapenzi wa soka kushuhudia mchezo mmoja kuchezwa katika dimba la Azam Complex Chamazi majira ya saa moja jioni kwa mujibu wa ratiba wakati Azam FC itakapo wakaribisha Kagera Sugar.

Michezo mingine ya Ligi Kuu inatarajiwa kuendelea tena hapo kesho tarehe 16 ambapo timu tano zikitarajia kuingia katika viwanja mbali mbali, Majimaji FC ikiwakaribisha mabingwa wa tetezi Yanga SC, Mtibwa Sugar ikicheza na Mbao FC,Tanzania Prisons ikikabiliana na wanakuchele Ndanda FC, Lipuli FC dhidi ya Ruvu Shooting huku Stand United chama la wana ikipepetana na Singida United.

Na hapo keshokutwa tarehe 17 timu ya Mbeya City ikiwa na kibarua kizito kwa kuingia uwanjani bila kocha wao, Kinnah F. Phiri waliyemtimua kufuatia matokeo mabovu wanayoyapata itakabiliana na Njombe Mji katika mchezo wa namba 23 utakao pigwa katikia dimba la Sokoine Jijini Mbeya ilhali Simba SC ikiwakaribisha Mwadui FC katika dimba la uwanja wa Uhuru.

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments