Michezo

Yanga SC wafikia hatua nzuri Jangwani (+Video)

Klabu ya Yanga imeanza matengenezo ya uwanja wake wa Kaunda uliopo makao makuu ya klabu hiyo eneo la Jangwani Jijini Dar es Salaam.

Kupitia ukurasa wao wa  Instagram Mabigwa hao watetezi wameweka video ikionesha ukarabati ukiendelea katika uwanja huo na kuandika”Nusu ya uwanja iko karibu kufikiwa“.

Uwanja wa Kaunda au kama wengi walivyozoea kuuita Jagwani ulijengwa mwaka 1973 kwa gharama ya tsh milioni 3 ambazo zilipatikana kwa michango kutoka kwa taasisi mbalimbali na wahisani wengine.

Mapema mwaka huu klabu ya Yanga iliwaomba pia wadau na mashabiki wake waichangie klabu hiyo ili kuukarabati uwanja huo wa kaunda pamoja na kujenga hosteli za kisasa za wachezaji. Tazama Video hiyo inayoonesha Greda likisawazisha vifusi vilivyokuwa vimemwagwa uwajani hapo kwa siku kadhaa zilizopita

https://www.instagram.com/p/BdIGo2KBBZd/?taken-by=yangasc

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents