Yanga SC wamepata ushindi mwembamba dhidi ya St Louis – Boniface Ambani

Straika wazamani wa mabingwa wa kihistoria wa ligi kuu soka Tanzania Bara Young Africans, Boniface Ambani amesema kuwa timu yake hiyo ya zamani kwa ushindi uliyo upata wa klabu bingwa Afrika dhidi ya St Louis ni mdogo mno na hivyo watakuwa na kibarua kizito katika mchezo wa marudiano.

Ambani ambaye ni raia wa Kenya ameyasema hayo wakati wa mahojiano kupitia kipindi cha michezo kinachorushwa na radio ya Magic FM.

“Yanga SC wameshinda ushindi mwembamba sana wa goli moja ila wakijitahidi huko ugenini watasogea mbele,” amesema ambani ambaye amewahi kuichezea Yanga SC msimu wa mwaka 2009/10.

Alipoulizwa na mtangazaji wa kipindi hicho juu ya mtazamo wa timu hiyo kwa sasa ligi kuu soka Tanzania Bara Ambani amesema “Huwa naifuatilia timu yangu naona Msimbazi wanashikilia msukani tu, Yanga SC wanashinda mara wanapoteza ndiyo mchezo.”

Boniface Ambani ambaye ni raia wa Kenya amewahi kuichezea Yanga SC msimu wa mwaka 2009/10 na kufanikiwa kufunga jumla ya mabao 18 katika michezo 24 aliyopata kucheza na kuipatia ubingwa wa ligi kuu soka Tanzania Bara kabla ya kutangaza kustaafu.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW