Michezo

Yanga SC watokea mlango waliotokea Azam FC, Matumaini yabakia VPL

Klabu ya Yanga leo Aprili 01, 2018 imejikuta ikitupwa nje ya michuano ya kombe la shirikisho (ASFC) dhidi ya Singida United baada ya kukubali kichapo cha goli 4-2 kwa changamoto ya mikwaju ya penati dhidi, baada ya timu zote kutoka sare ya goli 1-1 .

Katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo timu ya Yanga ilifanikiwa kupata bao lake la kwanza kupitia mchezaji wake Yusuf Mhilu kwa kutumia mpira wa kichwa akiunganisha kona ya Ibrahim Ajib Kayika katika dakika ya 23.

Kipindi cha pili, Singida United walifanikiwa kusawazilisha bao la Yanga kupitia mchezaji wao Kenny Ally na mpaka kipenga cha mwisho kinapulizwa timu hizo zilitoka sare ya goli 1-1. Hatua iliyopelekea changamoto ya mikwaju ya penati.

Kwa matokeo hayo, Singida United inasonga mbele kwenye hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo ambapo itavaana na JKT Tanzania.

Jana kwenye michuano hiyo, Klabu ya Azam nayo ilitupwa nje ya michuano hiyo kwa kukubali kipigo kutoka kwa mTibwa Sugar.

Timu ya Yanga kwa sasa itakuwa imebakiwa na taji moja mkononi inalowania kwa msimu huu wa 2018/19 baada ya kutolewa leo na Singida United kunako dimba la Namvua mjini Singida.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents