Michezo

Yanga SC yaifuata Simba SC kombe la Shirikisho Afrika

Yanga SC yaangukia katika michuano ya kombe la Shirikisho baada ya kutolewa klabu bingwa Barani Afrika dhidi ya Township Rollers FC huko nchini Botswana.

Yanga SC imeyaaga mashindano hayo baada ya kulazimishwa sare ya bila kufungana huku mchezo wa awali uliyopigwa jijini Dar es Salaam ilikubali kipigo cha mabao 2 – 1.

Yanga SC yakwea pipa kuwafuata Township Rollers ya Botswana

Kwa matokeo hayo sasa timu itatinga kombe la Shirikisho Barani Afrika  kutokana na matokeo yake iliyopata michuano ya klabu bingwa Afrika.

Township Rollers inafanikiwa kusonga mbele hatua ya makundi na kuweka historia hiyo baada ya kuwa na safari ngumu wakati ikiwa imekutana na Al Merkhe kabla ya kukutana na Yanga SC.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents