Michezo

Yanga SC yaishusha Simba SC kileleni, matokeo ya VPL

Ligi kuu Tanzania Bara imeendelea tena hii leo ikiwa ni mzunguko wa sita kwa michezo mitano kupigwa katika viwanja mbalimbali nchini lakini kubwa wapenzi wa soka walikua wakiangazia matokeo yatakayopatikana katika mchezo wa Kagera Sugar dhidi ya Mabingwa wa kihistoria klabu ya Young Africans.

Katika mchezo huo uliyopigwa guko Kaitaba mjini Bukoba Mabingwa watetezi klabu ya Yanga imechomoza na ushindi wajumla ya mabao 2-1 mbele ya mwenyeji timu ya Kagera Suger.

Mabao ya Yanga SC yakifungwa na Obrey Chirwa , Ibrahim Ajib huku la Kagera Sugar ikifanikiwa kupata bao la kufutia machozi kupitia kwa mchezaji Kibaya

Katika michezo mingine Mwadui FC ikiwa nyumbani imetoka sare ya 1-1 mbele ya Azam FC, wakati Ndanda FC nayo ikitoka sare 1-1 dhidi ya Majimaji FC, Ruvu Shooting ikitoka sare tasa ya bila kufungana dhidi ya Singida United huku mchezo watano ukiwa ni timu ya Mji Njombe ikitoka sare ya bila kufungana mbele ya Lipuli FC.

Haya ndiyo matokeo ya mechi zote zilizopigwa leo katika

Msimamo wa ligi baada ya mechi zote za leo umeiweka Yanga SC kileleni huku Kagera Sugar ikiendelea kuburuta mkia.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents