Michezo

Yanga Sc yamchapa Toto Africans bila huruma Taifa

By  | 

Klabu ya soka ya Dar es salaam Young African, imechomoza na ushindi mwembamba wa goli 1 kwa 0 dhidi ya klabu ya Toto Africans mchezo uliochezwa katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam

Mechi hiyo iliyokuwa na umuhimu mkubwa kwa pande zote mbili, Yanga inafakiwa kutetea ubingwa wake wa Ligi Kuu Bara. Yanga imefikisha jumla ya pointi 68 ambazo zitafikiwa na Simba iwapo itashinda mechi yake ya mwisho, lakini tofauti ya mabao 11 kati yake na Simba inawapa taji mapema.

Katika mchezo huo goli la klabu ya Yanga limefungwa na Mrundi Amisi Tambwe kunako dakika ya 81 ya mchezo,Vijana wa Mwanza Toto Africans walionekana kuamka na kutaka kusawazisha na kupiga mipira mingi iliyo lenga goli lakini bahati imeoneka kutokuwa yao na hivyo mchezo huo kumalizika kwa ushindi huo wa goli 1 kwa klabu ya Yanga huku Toto Africans wakiambulia patupu.

BY HAMZA FUMO

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments