Michezo

Yanga SC yavutwa shati na Mwadui FC uwanja wa Uhuru

Mchezo wa ligi kuu soka Tanzania Bara baina ya mabingwa watetezi klabu ya Yanga dhidi ya Nwadui FC umemalizika Uwanja wa Uhuru kwa timu hizo kutoka sare tasa ya bila kufungana.

Kwa matokeo hayo Yanga SC inasalia katika nafasi yake ya tano kwakuwa na ponti 22 wakati Mwadui FC ikiwa na alama 13 na kuzishusha Kagera Sugar, Ndanda FC na Mbeya City.

Michezo mingine ya ligi kuu inatarajiwa kupigwa hapo kesho ambapo vinara wa ligi Simba SC itakuwa mwenyeji kwa kuwakaribisha Singida United inayoshika nafasi ya tatu wakati Majimaji itakuwa mwenyeji dhidi ya matajiri wa Dar es Salaam wanalambalamba Azam FC wanaoshika nafasi ya pili mechi itayopigwa uwanja wa Majimaji.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents