Michezo

Yanga wajipanga kutwaa ubingwa leo

Kocha msaidizi wa Klabu ya Yanga, Juma Mwambusi ameizungumzia mechi ya leo dhidi ya Toto Africa kama mechi ya fainali kwao na wamejiandaa kuwakabili kwa kila namna ili wapate matokeo yatakayowapa ubingwa wa Ligi kuu.

Tokeo la picha la yanga
Kikosi cha Yanga

Mwambusi amesema wao kama benchi la ufundi wameiandaa vyema timu yao kucheza kwa ushindani ili washinde mechi hiyo na kujiweka katika mazingira mazuri ya kubeba ubingwa wa ligi kuu, huku akitoa angalizo kwa Toto Africa ambao wanahitaji alama tatu ili wasishuke daraja .

Tunatambua Toto kesho watacheza kwa tahadhari kubwa ili kupata ushindi lakini tumewaandaa vyema wachezaji kimbinu, kiufundi na kisaikolojia ili kushinda uchovu na kucheza kwa moyo wote ”Alisema Mwambusi.

Mwambusi alikwenda mbali zaidi kwa kusema anawafahamu Toto Africa watakuja kwa mchezo wa kuwashangaza wengi kwani wanapambana wasishuke daraja lakini wao kama Yanga SC wanalifahamu hilo na wana uzoefu nalo kama ilivyokuwa katika mchezo wao jumamosi dhidi ya Mbeya City na dawa ya kukabiliana nao wameshaipata.

”Tunafahamu watakuja kwa kukamia dhidi yetu na tumejiandaa vyema kiufundi kwa hilo. Kushinda mchezo wa kesho ni muhimu sana kwetu kuelekea ubingwa, hivyo tahadhari zote tumechukua ” alieleza Juma Mwambusi mara baada ya mazoezi ya asubuhi jana.

Yanga SC wanacheza na Toto Africa leo uwanja wa Taifa majira ya saa 10:00 jioni ikiwa ni mechi yao ya 29 kuelekea mwishoni mwa msimu na alama zao 65 kileleni mwa ligi kuu vodacom Tanzania Bara na endapo watashinda leo basi watatangazwa kuwa mabingwa wa Ligi kuu Vodacom Tanzania Bara kwani Simba hata wakishinda mchezo wake wa Mwisho bado atakuwa amezidiwa magoli na Yanga labda itokee miujiza ya Mungu washinde magoli zaidi ya 10.

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents