Michezo

Yanga wakabidhiwa kiwanja na RC Makonda chenye thamani ya tsh milioni 700 (Video)

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo Juni 21 amekabidhi eneo lenye ukubwa wa hekari 7 pamoja na hati ya umiliki kwa Klabu ya Yanga kwaajili ya ujenzi wa Uwanja na matumizi mengine ikiwa ni ahadi aliyoitoa wakati wa Hafla ya harambee ya Uchangiaji wa Timu hiyo.

RC Makonda amesema eneo hilo lina thamani ya Shilingi Milioni 700 ambapo lipo umbali wa Km 14 kutoka Daraja la Mwalimu Nyerere na umbali wa Mita 200 kutoka Barabara kubwa.

Akikabidhi eneo hilo RC Makonda ametaka uongozi wa Yanga kuanza kuliendeleza eneo hilo kwa kujenga Uwanja na miundombinu yote inayohitajika.

Wakipokea Eneo hilo, Viongozi wa Yanga,Bodi ya Wazamini na Mashabik wa Timu hiyo wamemshukuru RC Makonda kwa kuwapa eneo ambalo lipo kwenye mazingira mazuri ya tambarare na kuwatimizia ndoto waliyoishi nayo kwa miaka mingi bila mafanikio.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents