Michezo

Yanga wamkamata mnyama ‘Simba SC’ kwenye mbio za ubingwa wa VPL

Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya soka Vodacom Tanzania Bara klabu ya Yanga jana imefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ndanda FC kunako dimba la uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

Bao pekee la ushindi kwa Yanga lilifungwa na mshambuliaji wao Ibrahim Ajib dakika ya 34 kipindi cha kwanza.

Yanga sasa imefikisha pointi 8 sawa na mahasimu wao Simba ambao wote wamecheza mechi 4. Ingawaje Simba wanasalia katika nafasi ya pili kwa tofuati ya mabao ya kufunga na kufungwa huku Yanga ikiwa katika nafasi ya tatu wote wakisubiri matokeo ya klabu ya Azam FC .

Katika michezo mingine iliyopigwa jana Majimaji wakiwa nyumbani wamekubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Njombe Mji. Mwadui nayo imekubali kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa Tanzania Prisons ya Mbeya.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents