Habari

Yanga wamuweka roho juu Vincent Bossou

By  | 

Beki kisiki wa klabu ya Yanga, Vincent Bossou ameweka wazi kuwa atajua hatma ya maisha yake ndani ya kikosi hicho kama atakuwepo kwa msimu ujao au laa baada ya kurejea nchini akitokea mapumziko Dubai.

Vincent Bossou

Bossou ni miongoni mwa wachezaji wa kimataifa wa Yanga ambao wamemaliza mkataba kuitumikia klabu hiyo na mpaka sasa klabu hiyo imemchunia licha ya taarifa kusambaa kuwa anawindwa na klabu ya Singida United.

Mpaka sasa Bossou amesema hajafanya mazungumzo yoyote na uongozi wa Klabu ya Yanga hivyo hajui lolote kama atarejea tena kikosini hapo.

Sifahamu lolote kuhusu kurejea ndani ya Yanga kwa sababu sijaongea na viongozi tangu mkataba wangu ulipofika ukingoni, kwa sasa nawasubiri wao waniite ili tuanze kujadili juu ya mkataba mpya.“amesema Bossou huku akisisitiza kuwa yupo likizo kujifua

Muda huu nipo mapumzikoni nyumbani, najipa muda zaidi wa kukaa na familia sambamba na kufanya mazoezi ili msimu ujao niwe na kiwango kikubwa zaidi ya kile ambacho nilikionyesha msimu uliopita wa ligi,” amesema Bossou kwenye mahojiano yake na Gazeti la Championi.

Beki huyo ambaye tayari amepata ofa ya Klabu kubwa tatu kutoka ulaya huku timu moja tuu kutoka Tanzania, Singida United ndiyo imeonesha nia ya kumsajili.

By Godfrey Mgallah

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments