Yanga wapeni furaha mashabiki wenu – Abbas Tarimba (+Video)

Mkurugenzi wa Uendeshaji wa SportPesa Tanzania, Abbas Tarimba ambao ni wadhamini wa kuu wa klabu ya Yanga SC, amewataka mashabiki wa timu hiyo kununua jezi halisi ili kuiongezea pato Young Africans Sports Club. Tarimba pia amewataka Yanga SC kuwapa furaha mashabiki wao hasa kutokana na juu ya mafanikio ya klabu hiyo kutokana na usajili. ”Niwatakie kila lakheri Young Africans bila shaka na klabu nyingine katika ligi hii ambayo imeanza majuzi, na ninachotaka kimoja niseme ni kwamba wapeni furaha wapenzi wenu, wapeni furaha wananchi juu ya mafanikio ya Klabu hii kutokana na usajili na haya mambo mengine yanayofanyika.”

IMEANDIKWA NA HAMZA FUMO, INSTAGRAM @fumo255

 

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW