Michezo

Yanga yaandika ujumbe wa matumaini, ni baada ya vuguvugu la mgogoro dhidi ya Mabosi zao GSM

Mabingwa wa kihistoria wa ligi kuu soka Tanzania Bara, Young Africans Sports Club imewatoa hofu mashabiki kwa kuposti picha inayomuonyesha bosi wao GSM huku ikiandika ujumbe wenye kuleta matumaini.

Kupitia akaunti yao ya kijamii ya Instagram Yanga imeandika ”Daima furaha na Amani ya Wanayanga huletwa na wenye upendo wa dhati na timu yao. Tuendelee kuijenga Yanga SC.”

Siku za hivi karibu timu hiyo ya Wananchi imekubwa na jinamizi la kutokuelewana ndani ya uongozi hadi kupelekea wengine kuchukuliwa hatua za kinidhamu kama vile Said Rupia na Frank Kamugisha huku wengine wakijiuzulu yote yakiibuka baada ya kuenea kwa taarifa za mdhamini wa klabu hiyo GSM kutangaza kupunguza majukumu yake kwa Wanajangwani hao

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents